HOTUBA YA MWENYEKITI WA BAVICHA KILIMANJARO WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI KATA YA NJORO. MANISPA YA MOSHI.
Posted in
Siasa
No comments
Monday, December 1, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Tunaanza rasmi kampeni leo- Novemba,30 2014 kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Desemba 14, 2014.Hii fursa njema kwa ajili ya kuwachagua viongozi tutakao shirikiana nao katika maeneo tunayoishi katika kuleta maendeleo.
Desemba 14,ni siku yenye fursa ya pekee kwa watanzania wote.Ni siku ya kuamua.Ni siku ya kuhukumu.Ni siku ya kutoa ujumbe wa kukataa ghiliba na hila za watawala wa CCM.Siku ya kutocheza na nyani ili kuvuna mabua.
Ni siku ya kuamua aina,sifa na hulka ya viongozi wanaofaa kutumikia wananchi.Ni siku ya hukumu ya viongozi wazembe na wasio wadilifu wa chama tawala. Ni siku ya kutoa ujumbe wa wazi kwa chama tawala kwa kuwa Kimechokwa na watanzania.
Hivi sasa taifa linayumba kutokana na kukosekana kwa viongozi wenye sifa za uadilifu na uaminifu ndani ya chama tawala.Hili linathibitishwa na mtiririko wa matukio yanayojirudia ya uzembe,ufisadi na wizi wa mali za umma. Viongozi wa CCM wanaliongoza taifa kwenye mzunguko wa Ufisadi.Ufisadi umeaanzia ndani ya chama tawala.
Mwaka 2010,Yussufu Makamba, aliyekuwa katibu mkuu wa CCM,alipokea malalamiko ya rushwa wakati wa kura za maoni ndani ya chama hicho, alisema kwamba wagombea wote walitoa rushwa,ila walizidiana kwa viwango tu.
Kwa kutoa Kauli hii,makamba alimaanisha,wagombea walioshindana kutoa rushwa ili kupata ridhaa ya kugombea,wakipewa dhamana ni ruksa kushindana kupiga dili za kifisadi pesa zao zirudi.
Pengine,Makamba anakijua Chama cha mapinduzi,kuliko mimi mwenyekiti wa vijana.Hali halisi ndio hiyo. Sote tunajua, chama cha wala rushwa na mafisadi huzaa serikali ya walarushwa na mafisadi.Mwaka 1995,baba wa taifa,hayati Julius Kambarage Nyerere aliona haya,alisema kwamba CCM ya sasa inanuka rushwa na ufisadi.Alisema chama legelege huzaa serikali legelege.Serikali ya wala rushwa na mafisadi haikusanyi kodi.Ni serikali inayobariki ufisadi wa kila namna.
Kuna mifano;
Mwaka 2005,makampuni yenye uhusiano na chama tawala yalichota bilioni 133.Fedha hizi zilitumika kwenye uchaguzi mkuu wa 2005.CCM ilitumia fedha nyingi kushinda huku ikiahidi maisha bora kwa kila mtanzania ambayo mpaka leo hakuna.Ni maisha duni kwa kila mtanzania.
Mwaka 2013, ilibainika kuna mafisadi serikali na ndani ya chama tawala wametumia mwanya serikali legelege kutorosha kwenda Uswisi zaidi ya bilioni 300(maarufu kama mabilioni ya uswisi.Serikali ya CCM haina mpango wa kuchukua hatua zozote.Kila mbinu imefanyika ili kulinda wezi hawa.
Mwaka huu,imefichuka zaidi ya bilioni 300 za kwenye akaunti ya Tageta Escrow zimechota kifisadi na watawala.Mpango huu wa kifisadi umefanyafika mbele ya macho na baraka za viongozi wa serikali.
Hii ndiyo hulka ya CCM,ndio hulka ya wagombea wa CCM.Kuna taarifa kwamba CCM inaandaa mpango hatari wa kutumia uongo,ghilba,fedha mgao wa escrow, hila na mbinu chafu ili kushinda uchaguzi huu.
Kwa hali hii,inawezekana CCM ikatengeneza mpango ufisadi wa Escrow kwa kila mtaa ili kugawana fedha za walipa kodi.Jamani! tuko tayari kuchagua viongozi watakaotengeneza escrow kwenye mitaa wa njoro…….?
Kwetu chadema,tunapozungumzia uchaguzi,tunazungumzia wagombea waadilifu,waaminifu,wenye, uwezo,wanaojua matatizo ya yenu,wawajibikaji na wenye upendo kwenu.
CCM,wanapozungumzia uchaguzi,wanazungumzia mgombea aliyefuzu katika mashindano ya mgao wa fedha wakati wa kura za maoni.Lengo ni kupata kiongozi wa kutengeneza dili za EPA,Escrow na Richmond katika ngazi ya mitaa.
Tunaweza kuepuka balaa hili kwa kutopigia wagombea wa CCM.CCM iko tayari kulinda wezi walioiba pesa za EPA,mabilioni ya uswisi,mishahara hewa na akaunti ya “Tageta Escrow” hata kama ikibidi watanzania kwenye mitaa mbalimbali nchini waendelee kula nyasi,kufa kwa kukosa dawa hosptalini na kunywa maji machafu na kukosa mikopo(wanafunzi),kujifungulia barabarani (wanawake)
Nahitimisha kwa kusema kwamba tukitokeze kwa wingi kupiga kura za kukataa CCM ili kuthibitisha kuwa nchi hii sio mali ya ccm na viongozi wake bali ni mali ya wanyonge(wakulima,wafanyakazi, Wafanyabiashara wadogo n.k) wa Tanzania.
Tujitokeze kwa wingi kupiga kura za kuikataa CCM ili iwe hukumu na ujumbe mahususi wa serikali ya kifisadi CCM kwamba sisi wananchi tunachukizwa na dili za kifisadi zinazotekelezwa mbele ya macho ya serikali ya CCM.NI Uchaguzi wa kukataa mafisadi na ufisadi.
Wagombea kupitia chadema waliopo mbele yenu, ni waaminifu wazalendo,wachapa kazi,wawabikaji,wanayajua matatizo yenu,wana uwezo,ni wazalendo na wako tayari kuwatumikia.Wapeni kura zenu ili wawatumikie kwa muda wa miaka minne ijayo.
Asanteni.
KIBONA DICKSON.
MWENYEKITI BAVICHA KILIMANJARO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :