MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA MTANDI NA MWENGE HUKO LINDI MJINI
Posted in
Siasa
No comments
Saturday, December 6, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mtandi iliyoko Lindi Mjini wakati alipotembelea Kata hiyo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha Lindi mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha ishara ya vidole viwili kuashiria kuunga mkono pendekezo la muundo wa serikali mbili nchini wakati alipozungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi tarehe 5.12.2014.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
Baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini Mama Salma Kikwete anaonekana akimbeba mtoto Juma Selemani ambaye naye alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa kampeni.PICHA NA JOHN LUKUWI.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :