MPAKISTANI ALIYETOROSHA TWIGA JELA MIAKA 60, WATANZANIA WAACHIWA HURU

No comments
Saturday, December 6, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu, Moshi

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro, jana imemhukumu miaka 60 jela, mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya Utoroshaji wa wanyama hai 153, wakiwemo Twiga 4, Mpakistani Kamran Ahmed na kuwaachia huru Watanzania watatu.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo alisema baada ya upande wa Jamhuri kufanikiwakujenga kesi dhidi ya mpakistani huyo, kwa kiwango kisicho acha mashaka, Mahakama yake Imeridhika kwamba Mpakistani huyo alitenda makosa yote manne yaliyowasilishwa dhidi yake.

Kobelo alisema Mahakama hiyo pia inaawachia huru Watanzania watatu, Hawa Mang’unyuka, Mathew Kimathi na Michael Odisha Mrutu kwa sababu Jamhuri imeshindwa kujenga kesi dhidi yao na hata ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo haoneshi kuwaunganisha washitakiwa hao moja kwa moja na kosa la kusafirisha wanyama hai nje ya nchi.

Katika hukumu hiyo, Kamran alikutwa na makosa manne, kushiriki na kula njama ya kutenda uhalifu kinyume cha kifungu 57 (1), sehemu ya 4(1), sura ya kwanza ya kosa la uhujumu uchumi na kushiriki utoroshaji wa wanyama hai wenye thamani ya shilingi milioni 170, 575,500.

Kosa la pili ni kufanya biashara ya kukamata na kusafirisha wanyama hai wakiwemo Twiga, Chui, ndege wa aiana mbalimbali, Duma, Nyati, Pofu, Punda milia na Swala, bila
Leseni, kosa la tatu ni kukutwa na Nyara za Serikali katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tukio lililotokea Novemba 26, mwaka 2010 na kosa la nne ni la kuisababishia serikali hasara ya Dola 113.7 kwa kufanya biashara kinyume cha sheria.


Kuhusu kumuachia Huru Mshitkakiwa Namba mbili, Hawa Mang’unyuka ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Harm Marketing na Luwego Bird Trappers, inayodaiwa leseni yake kutumika kuhalalisha ukamataji na utoroshaji huo, Hakimu Kobelo alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa ni wazi kwamba Kampuni ya Mshitakiwa namba mbili (HAWA), ilipewa kibali halali ya kukamata wanyama hai na mamlaka husika hivyo Mahakama hiyo inashindwa kumtuhumu moja kwa moja na utoroshaji huo.

“Ukirudi kwa mshitakiwa wa pili, jibu liko wazi, Hawa Mangunyuka kupitia kampuni yake ya Harm Marketing alikuwa na leseni za kufanya biashara ya kukamata wanyama, baadae kupitia mamlaka hizo hizo ziliruhusu mshitakiwa wa kwanza kufanya biashara hiyo hiyo kupitia Harm Marketing na katika kipindi hicho, Kamran aliendelea kutumia leseni hiyo mara kwa mara,” alisema Kobelo.

Kwa upande wao washitakiwa wa 3 na 4, Mathew Kimathi na Michael Mrutu, kwa sababu hakuna sehemu yoyote inayoonesha ushiriki wao katika utoroshaji zaidi kutekeleza wajibu wao kama walivyoekezwa na wakuu wao wa kazi kipindi hicho.

Novemba 26, mwaka 2010, Kamran anadaiwa kuwatorosha wanyamka hai 153 wakiwemo Twiga 4, kwenda Doha Qatar kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kutumia ndege ya Kijeshi, namba C17, kinyume cha kinyume cha kifungu namba 84(1) cha sheria namba 5 ya uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 2009.


Mwisho.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .