IRAQ YASEMA HAISAIDIWI KUKABILI ISIS
Posted in
International
No comments
Tuesday, June 2, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Hatusaidiwi
vya kutosha ,hayo ni maneno yake waziri mkuu wa Iraq ,Haider al-Abadi.
Anasema kuna ushahidi mdogo sana wa kuwepo kwa uungwaji mkono wa
kimataifa katika vita vyao dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika
nchi yake Iraq.
Bw. Haider al-Abadi, ameonya kuwa kinyume na matarajio wanamgambo hao wa ISIS wanaendelea kuwasajili watu wengi kujiunga nao. Matamshi
hayo ya Bwana Abadi yanakuja wakati wa kikao kinachotarajia huko
Ufaransa cha mataifa yaliyoungana kuipiga vita Islamic state.
Mawaziri wa maswala ya kigeni
kutoka nchi hizo 20 wanakutana kujadili mikakati yao dhidi ya wanamgambo
wa Islamic State walioko Iraq na Syria. Mwandishi wa BBC aliyeko
mjini Paris anasema kuwa kutekwa kwa Ramadi na wapiganaji wa Islamic
State kumeashiria kushindwa kwa mkakati uliopo sasa na kuongezeka kwa
utegemezi wa Iraq kwa wanamgambo wa Shia wanaoungwa mkono na Iran .
Waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ni mmoja wa washiriki wa mazungumzo hayo. Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amesitisha wizara yake baada
ya kuvunjika mguu wake alipokua akiendesha baiskeli
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :