MWILI WA MAREHEMU MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA WAPOKELEWA BUKOBA, MAJONZI YATANDA KWA WANABUKOBA.
Posted in
Kifo
No comments
Tuesday, June 2, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Gari maalum kutoka Nchini Uganda lililobeba Mwili wa Mzee Samwel Ntambala Lwangisa ukiingia Bukoba.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Mwili
wa Marehemu Samuel Ntambala Luangisa uliwasili usiku wa kumkia leo
katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Mauti yalimkuta akiwa Nchini
Marekani na maziko yake itakuwa kesho jumatano june 3,2015. Wakati wa
Uhai wake Marehe Samwel Luangisa aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa
Mkoa wa Kagera (ukiitwa ziwa magharibi), Aliwahi pia kuwa mbunge wa
Bukoba Mjini, Meya wa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kitendaguro hadi mauti
yalipomkuta.
Mtoto wa Marehemu Bi. Murungi
Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis Kagasheki
Ni majonzi na huzuni
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :