KENYA: VIDEO YA WAPENZI WA JINSIA MOJA MARUFUKU!
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, February 24, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Bodi ya kudhibiti video na filamu nchini (KFCB) imepiga marufuku video moja ya muziki inayotetea haki za wapenzi wa jinsia moja.
Bodi hiyo inasema kuwa video ya ''wimbo huo inakiuka maadili ya jamii''
Wimbo huo wa "Same Love (Remix)" ni chapa ya wimbo wa awali ulioimbwa na Macklemore na Ryan Lewis mwaka wa 2012.
"Same Love'' unatambulishwa kama wimbo unaotetea maslahi ya wapenzi wa jinsia moja katika anuani yake ya mtandao wa video wa Youtube.
Katika video hiyo iliyochapishwa yapata juma moja lililopita na kutazamwa na takriban mara elfiu arobaini katika mtandao wa Youtube.
Haijulikani kwa njia gani bodi hiyo itatekeleza marufuku yake.
Mkurugenzi wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alitangaza marufuku hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.
Habari Zingine
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :