AFRIKA MASHARIKI: HATMA YA WAKENYA WALIOFUNGWA NCHINI TANZANIA KUJULIKANA IJUMAA HII

No comments
Thursday, March 17, 2016 By danielmjema.blogspot.com

MAHAKAMA ya Afrika inayoshughulikia haki za binadamu, iliyoko jijini Arusha, nchini Tanzania inatarajiwa kutoa hukumu yake kuhusu hatma ya Wakenya 10 ambao wameistaki serikali ya Tanzania. wakidai iliwakamata kimakosa wakiwa Maputo, Msumbuji.

 
Afisa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya mahakama hiyo, Sukhdev Chhatbar alisema kuwa katika shitaka namba 006/2013, Wilfred Onyango na wenzake dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, itasikilizwa siku ya ijumaa, machi 18 mwaka huu, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Wakenya hao, ambao wamekuwa wakitmikia kifungo kwa zaidi ya miaka 10 sasa katika magereza ya Tanzania, wamedai kuwa Januari 16, mwaka 2006, walikamatwa kimakosa wakiwa katika shughuli zao halali za kibiashara nchini Msumbiji, kisha wakabambikiwa kesi ya mauaji na mashitaka matatu ya wizi wa kutumia silaha kitendo.

Katika kikao chake cha kawaida cha 37, jopo la majaji waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo wakati huo, kati ya walalamikaji (wakenya) dhidi ya Jamhuri, Mei 2015, walielezwa na Upande wa Jamhuri kuwa, Wakenya hao walikamtwa katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, wakitokea nchini Msumbiji baada ya kuletwa na ndege ya kijeshi ya Msumbiji.


Wakenya ambao wamekuwa wakitumikia kifungo cha miaka 30 jela katika ardhi ya Tanzania ni pamoja na  Wilfred Onyango Nganyi 'Dadii', Peter Gikuru Mburu, 'Kamau', Jimmy Maina Njoroge, 'Ordinary' na  Patrick Mutheee Muriithi, 'Musevu'.

Wengine ni, Simon Githinji Kariuki, Boniface Mwangi Mburu, 'Bonche', David Ngigu Mburu, 'Mike', Gabriel Kungu Kariuki na Simon Ndungu Kiambuthi, 'Kenen' ambapo watuhumiwa wengine wawili Peter Kariba na John Odongo Odhiambo, walipoteza maisha kabla ya hukumu kutolewa. Mahakama hiyo inaundwa na jopo la majaji 11 kutoka katika mataifa wanachama wa umoja wa Afrika (AU).

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .