KENYA: RAIS KENYATTA AIANGUKIA CORD; AITAKA IACHE UBINAFSI WA KISIASA

No comments
Wednesday, March 16, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, ameitaka chama kikuu cha upinzani, muungano wa CORD, kuachana na siasa za ubinafsi yenye mrengo wa kujipendelea. Akizungumza na mamia ya wakazi wa Eldama Ravine, siku ya Jumatano, Machi 16, mwaka huu, Rais Kenyatta alisema kuwa viongozi wa CORD, wakiongozwa na Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga, wamekuwa wakitoa matamshi ambayo yanalenga kuchochea chuki kwa lengo la kusababisha migawanyiko nchini.

Msafara wa Rais Kenyatta katika Kaunti ya Baringo mapema leo, Machi 16, mwaka 2016

Rais Kenyatta, aliendelea kwa kusema kuwa,  muungano huo, umeachana na utamaduni umoja na mshikamano ulioasisiwa na Rais Mstaafu, Mwai Kibaki pamoja na Waziri mkuu Mstaafu, Raiala Odinga, mwaka 2007 na badala yake wanachokifanya sasa hivi ni kuchochea migogoro na mparanginyiko wa kitaifa.


Katika mkutano huo, Rais Kenyatta alitoa wito kwa vyama tanzu vinavyounda muungano wa Jubilee, kuona umuhimu wa kuungana na kuwa kitu chini ya mwavuli wa chama kimoja wa Jubillee kama njia pekee ya kuimarisha umoja wao kuelekea uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwakani.

“Tuliafikiana kuwa kipaumbele chetu kama Jubilee ni Amani na mshikamano, Uhasama hauwezi ukaleta maendeleo lakini endapo tutaungana na kuwa kitu kimoja (chama kimoja), tutafanikiwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo kama Taifa,” alisema Rais Kenyatta.

Aidha, Rais Kenyatta alitumia fursa hiyo, kutoa ufafanuzi kuhusu safari za mara kwa mara nje ya nchi, safari ambazo zimekuwa zikipingwa na upinzani, ambapo alisema kwamba, Serikali ya Jubilee imefanikiwa kupata msaada wa kifedha ambayo imeelekezwa katika miradi ya kimendeleo nchi nzima.

 “Wanasema nasafiri sana, hawajui sababu za safari zangu, lakini napenda kuwambia kuwa serikali yangu imefanikiwa kufanya mengi kutokana na msaada ya nchi wahisani, pesa ambayo tumeielekeza katika kaunti ya Baringo pekee kwa mfano, ni Ksh 12.2 bilioni, hiyo pesa imetoka wapi?" alihoji Rais Kenyatta.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais, William Ruto, alivitaka vyama vyote vinavyounda muungano wa Jubilee kuvunja vyama vyao na kuungana na chama cha Jubilee (JAP) na kuongeza kuwa kwa kuingia katika uchaguzi mkuu ujao chini ya chama kimoja, kutawahakikishia ushindi wa kishindo.

Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, wapo katiika ziara ya kiserikali katika kaunti za Nakuru na Baringo ambapo wakati ni wazi kuwa Rais atatumia ziara hizo kukagua miradi ya maendeleo, pia atatumia fursa hiyo kuhamasisha Wakenya kumuunga mkono, kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .