ARSENE WENGER AJITETEA BAADA YA KICHAPO CHA BARCELONA

Posted in
No comments
Thursday, March 17, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini vijana wake walicheza vyema uwanjani Nou Camp licha ya kulazwa 3-1 na Barcelona Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Arsenal walilazwa kupitia mabao ya Neymar, Luis Suarez na Messi. Bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Mohamed Elneny.


Arsenal hawajafika hatua ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu 2010. "Nafikiri tulicheza vyema, ulikuwa mchezo mzuri kati ya timu mbili nzuri. Tumeondolewa kwa masikitiko lakini wana ustadi wa hali ya juu hasa katika safu ya mashambulizi na ukifanya kosa kidogo tu safu yako ya ulinzi wanaweza kukuadhibu,” alisema Wenger baada ya mechi.

"Wakati muhimu katika mchezo huo ni mambo yalipokuwa 1-1 kwa sababu nilidhani walikuwa wanayumbayumba kiasi. Kama tungefunga bao la pili wakati huo badi mambo yangekuwa tofauti labda. Lakini hatukuweza.

"Katika michezo yote miwili, ukiangalia nafasi ambazo tuliunda, zilikuwa nyingi. Inauma kuondolewa kwenye michuano lakini tulicheza vyema sana dhidi ya timu ambayo labda ndiyo bora zaidi Ulaya.” Arsenal walilazwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza uwanjani Emirates, mabao yote yakifungwa na Lionel Messi.


Arsenal sasa watajaribu kufufua kampeni yao msimu huu kwa mechi ugenini Goodison Park dhidi ya Everton Jumamosi. Barca, watakaokutana na Villa Real ligini Jumapili, watajua mpinzani wao robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Ijumaa droo itakapofanywa mjini Nyon, Uswizi.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .