RIPOTI: DONALD TRUMP AKIWA RAIS DUNIA HAITOKUWA SALAMA
Posted in
Kimataifa
No comments
Thursday, March 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Shirika moja la kimataifa limesema
ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu
zaidi zinazokabili dunia. Shirika hilo la Economist Intelligence
Unit linaonya kuwa iwapo Bw Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda
likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama
dhidi ya Marekani.
Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Bw Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Bi Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema "ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic".
Ushindi wa Trump unaorodheshwa kuwa hatari zaidi kwa dunia kushinda hata Uingereza kuondoka kutoka kwa Umoja wa Ulaya au hata makabiliano ya kivita katika bahari ya South China Sea. Kuyumba kwa uchumi wa Uchina au Urusi kuingilia kivita Ukraine na Syria na kusababisha “vita baridi” vipya ni miongoni mwa mambo ambayo yanachukuliwa kuwa hatari zaidi ya ushindi wa Bw Trump.
"Kufikia sasa, Bw Trump ametoa maelezo machache sana kuhusu sera zake, na huwa anabadilisha sana msimamo wake,” EIU wanasema kwenye ripoti yao ya utathmini wa hatari zinazokabili dunia. Utathmini huo huangazia pia athari za jambo fulani na uwezekano wa jambo hilo kutokea.
- Al-Shabab wamtumia Trump wakitafuta wafuasi
- US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
- Adele:Trump hana idhini ya kutumia nyimbo kisiasa
Bw Trump amependekeza ua ujengwe kati ya Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji na pia ametetea kuuawa kwa jamaa za magaidi. Aidha, amependekeza kuvamiwa kwa Syria ili kuangamiza kundi la Islamic State.
EIU wanasema pendekezo msimamo wake kuhusu mzozo Mashariki ya Kati pamoja na pendekezo kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani vinaweza kutumiwa na makundi ya itikadi kali za Kiislamu kuwatafuta wafuasi zaidi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :