CHINA: WATU 300,000 WAADHIBIWA KWA UFISADI

Posted in
No comments
Monday, March 7, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais wa China, Xi Jin Ping
Chama tawala cha Kikomunisti nchini Uchina kimesema maafisa karibu 300,000 wa chama hicho waliadhibiwa mwaka jana kwa tuhuma za ufisadi. Maafisa 200,000 walipewa kilichodaiwa kuwa “adhabu ndogo” huku wengine 80,000 wakipewa adhabu kali.

Rais Xi Jinping amefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa ajenda kuu ya utawala wake. Maafisa wakuu wa kisiasa wamefungwa jela baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.

Kila siku, ni kama kawaida kupata habari za maafisa wa serikali waliochunguzwa au kuadhibiwa kwa sababu ya ufisadi, kutumia vibaya mamlaka au tuhuma nyingine zinazohusiana na ulaji rushwa.

Idadi ya walioadhibiwa mwaka 2015 ilitangazwa wakati wa kikao cha kila mwaka cha bunge la Uchina. Mtathmini wa BBC anayehusika na masuala ya Uchina anasema tangazo hilo linaonekana kama onyo kwa wajumbe wa chama waliokusanyika Beijing kwamba chama hicho kitaendelea kuwaadhibu maafisa wafisadi.

CHANZO: BBC SWAHILI

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .