KENYA: KERICHO NA MALINDI WAAMUA, KATIKA UCHAGUZI MDOGO

No comments
Tuesday, March 8, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mgombea wa Jubillee, Aaron Cheruiyot, ameibuka mshindi wa kiti cha senate, katika uchaguzi mdogo, kwenye kaunti ya  Kericho iliyofanyika jana, akijizolea jumla ya kura 109,358 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Paul Sang wa Kanu aliyeambulia kura 56,307. na hivyo kutangazwa na tume huru ya uchaguzi, IEBC, kuwa Seneta mpya wa Kaunti hiyo.
 
Ushindi wa Cheruiyot, unatafsiriwa kama sababu ya kukenua kwa Makamu wa Rais. William Ruto ambaye uchaguzi huo, ulionekana kama kipimo cha umwamba katika siasa za bonde la ufa.

Licha ya ushindani mkubwa uliojitokeza kipindi cha kampeni, Cheruiyot alifanikiwa kumgaragaza Sang katika uchaguzi huo ambao ulishuhudia jumla ya wagombea sita wakijitokeza, huku kukiwa na idadi ya wapiga waliojitokeza ukikasimiwa kuwa ni asilimia 58 pekee.

Matokeo ya wagombea wengie ni kama ifuatavyo, Daniel Tonui (NVP), alipata kura 772, Wycliffe Kipkemoi Ngenoh wa MDP (497), Paul Kipyegon Sigei wa UDM  (473) na David Kipkoech Mutai wa  ND alipata kura 427.
 

Wakati huo huo, katika uchaguzi mdogo wa ubunge mjini Malindi, Mgombea William Baraka Mtengo wa Orange Democratic Movement (ODM), ndiye mbunge mpya, akijipatia kura 15,582 na kumbwaga mpinzani wake wa karibu, Pihilip Charo wa Jubilee, aliyepata kura 9,243.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .