MICHEZO: FRANK NUTTAL AIHAMA GOR MAHIA.

No comments
Monday, March 7, 2016 By danielmjema.blogspot.com

KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Kenya (KPL), Mskochi, Frank Nuttal, ameigura klabu hiyo ambapo taarifa za awali zinasema kuwa, Kocha huyo, amehamia Zamalek ya Egypt.

Nuttal ameondoka klabuni hapo, siku moja baada ya kujikuta rekodi yake ya kutokupoteza mchezokatika kipindi cha miezi 17 mfulululizo,  ikivunjwa walipokubali kichapo cha goli 1-0, kutoka kwa mahasimu wao, AFC Leoapards, katika mchezo wa ligi kuu msimu "Mashemeji Derby" uliopigwa siku ya jana, Machi 6, kwenye dimba la Kasarani, Jijini Nairobi.

Kwa sasa mskochi huyo ambaye aliipa ubingwa K'Ogalo msimu uliopita ikiwa ni taji lao la 15, hayupo nchini ambapo taarifa zinasema kuwa tayari yupo nchini Egypt ambapo ameenda kumalizia mazungumzo ya kuhamia katika Klabu ya Zamalek atakapohudumu kama kocha msaidizi chini ya Mskochi mwenzake,  Alex McLeish.

Nuttal amekuwa nawakati mgumu msimu huu, kutokana na kushindwa kupata ushindi na timu yake,ambapo katika michezo minne waliyoingia dimbani, wamefanikiwa kuvuna pointi tatu pekee, huku wakifunga goli moja tu jambo ambalo sio la kawaida.

Mbali na michezo ya Ligi, K'Ogalo pia ilijikuta ikibwagwa katika michuano yaKlabu Bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha 2-1 nyumbani na 1-0 ugenini dhidi ya mabingwa wa DRC, timu ya FC Lupopo.

Kama hiyo haitoshi, Nuttal alimanusura aoneshwe mlango wa kutokea , siku chache kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi mwaka huu, ambapo jaribio la kumtimua kazi lilisitishwa baada ya Jeshi la Kijani (Masabiki) kuingilia kati.

Wakati huo huo, taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinadai kuwa, Kocha Antonio Flores, Raia wa Hispania, yupo mbioni kurithi mikoba ya Frank Nuttal kama Kocha mkuu wa Gor Mahia.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .