UGANDA: MBAMBAZI APINGA USHINDI WA MUSEVENI KORTINI

No comments
Tuesday, March 1, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu uliomalizika majuzi Uganda, Amama Mbabazi ameiomba mahakama nchini humo ifutilie mbali ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu uliokamilika majuzi.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Kampala Uganda Patience Atuhaire anasema kuwa wakili wa waziri mkuu wa zamani Severino Twinobusingye aliwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya juu mwendo wa saa kumi na moha na dakika tano.

Waziri huyo mkuu wa zamani alimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya mshindi rais Yoweri Museveni na kiongozi wa chama cha upinzani FDC kanali mstaafu Kizza Besigye.

Ilitarajiwa na wengi kuwa kanali mstaafu Kizza Besigye ndiye angekata rufaa lakini hakuweza kufanya hivyo baada ya kuzuiliwa na polisi. Besigye amekamatwa mara 8 katika siku 10 zilizofuatia tangazo la ushindi wa rais Yoweri Museveni.

Kwa sasa kiongozi huyo wa FDC amezuliwa nyumbani kwake na hata jaribio la viongozi wa chama chake wakiongozwa na meja jenerali Mugisha Muntu kumtembelea nyumbani kwake halikufua dafu. Jenerali Mugisha ameahidi kukutana na wanahabari hapo kesho huku ikifahamika kuwa wameshindwa kuwasilisha rufaa mahakamani kaatika muda unaoruhusiwa na katiba ya taifa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .