UTAFITI: ASILIMIA 26.5 YA WANAWAKE HUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE NCHINI TANZANIA

No comments
Tuesday, March 29, 2016 By danielmjema.blogspot.com

UTAFITI mpya unaonesha kwamba, asilimia 26.5 ya wanawake nchini Tanzania, hufanya ngono kinyume na maumbile. Mtafiti Mwanasayansi Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia 26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume.

Baadhi ya wanawake kutoka Kinondoni Dar es salaam, Tanga, Makete na Siha wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile ambapo Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.


Amekaririwa akisema " Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi,wahudumu bar, wauguzi, makahaba naakina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo"


Wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambapo Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.


Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ni hafifu kwani wakitumia mipira (Condom) inapunguza raha. 


Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana akiuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.

Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana, wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .