GUMZO: JUKWAA KUANGUKA RAILA AKIWA ANAHUTUBIA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Tuesday, March 29, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Video inayoonesha kiongozi wa
upinzani Kenya Bw Raila Odinga na viongozi wengine wakianguka baada ya
jukwaa kuporomoka akihutubia mkutano wa hadhara imevuma sana mtandaoni
Kenya.
Bw Mtengo alishinda uchaguzi huo. Ilikuwa siku moja kabla ya Ijumaa Kuu na Bw Odinga alikuwa akisimulia kuhusu mateso aliyopitia Yesu Kristo.
“Wakati huu mimi nilikuwa nimeenda kule Jericho, nikaonyeshwa ile mlima ya majaribio. Pale ambapo shetani alimpeleka Yesu akamuonesha ulimwengu wote. Akamwambia angalia hii yote. Ukikubali kusujudu na kuniabudu hii yote itakuwa ni yako. Lakini Yesu akamwambia wewe nenda mbali shetani ..” alisema Bw Odinga kabla ya jukwaa kuanguka.
Video hiyo imesambazwa sana mtandaoni. Bw Odinga alikuwa ziarani Israel mapema mwezi huu.
Naibu mwenyekiti wa chama cha ODM eneo la Kilifi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation la Kenya akisema hakuna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho. Anasema watu waliokuwa kwenye jukwaa walipunguzwa na Bw Odinga akaendelea kuhutubia mkutano huo.
Habari Zingine
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :