CHOMBEZO LA WIKENDI: NJIA HIZI HUSAIDIA KULETA NURU KWA MPENZI WAKO
MAHUSIANO mwngi yamekuwa yakikumbwa na migogoro ya mara kwa mara. migogoro hii wakati mwingine huwa
inapelekea mapenzi baina ya wawili wapendanao kuchuja. Kuchuja huku kwa
mapenzi si kwamba ni tukio ambalo huwa linafurahiwa sana na wahusika,
hapana.
Bali hujikuta tayari kuwa limetokea kutokana na nafsi zao zenyewe
kuwa zimechoshwa na maudhi pamoja na kero za mara kwa mara katika
mahusiano. Kwa bahati mbaya kwa wengi hali kama hii inapowatokea huwapelekea
hata wenyewe waanze kuchokana na hatimaye kuachana hali ya kuwa bado
wanakuwa na chembe chembe hai za upendo katika mioyo yao. Haitakiwi kuwa
hivyo.
Migogoro katika mahusiano si kitu kigeni, huwa inatokea. Kitu cha
msingi ni kujua namna ya kufanya kuweza kutibu majeraha yanayoachwa na
migogoro katika mapenzi. Kwa kuzingatia hilo na mengine mengi hapa leo utaenda kukutana na
njia za kufanya ili uweze kulipa penzi lako uhai zaidi. Njia za uhakika
na zenye majibu chanya kwa wenye kuzifuata vile inavyotakiwa.
Hapa kuna njia za kufanya katika kulipa uhai penzi lenu kabla hali
haijawa mbaya zaidi na kufanya mkatengana hali ya kuwa bado mnapendana.
haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia katika mahusiano
Kuwa muwazi katika Mawasiliano
Asilimia nyingi ya migogoro katika mahusiano mengi huwa inasababishwa
na vyanzo vya mawasiliano simu ikiwa ndiyo kiongozi wao. Mahusiano
mengi yanaangamizwa na simu.
Japo kweli kuna baadhi ya watu huwa wanatumia simu katika kutenda
usaliti (kuwasiliana na mahawara zao), lakini mara nyingine simu huwa
inahusishwa katika matukio ya namna hiyo hata bila kushiriki. Kufanya
mawasiliano kwa kuonekana kukwepa mpenzi wako kusikia kile
unachozungumza hufanya ionekane kama usaliti unatendeka. Kitu ambacho si
sahihi sana.
Hivi ni kweli kila anayeenda kuzungumza na simu pembeni huwa anaongea na hawara yake? Si kweli. Kuna wengine huwa inawalazimu kufanya hivyo kutokana na sababu
tofauti ikiwemo kuongea mipango ya siri ya kikazi, mazoea ya kufanya
hivyo au kupata utulivu zaidi wa kuongea. Lakini ni mara chache sana
mpenzi wako kumueleza sababu hizi na akaonekana kukuelewa.
‘Nature’ ya mapenzi ilivyo ni kuaminiana na kuthaminiana. Sasa vipi akuelewe kwa sababu hizo? Ni ngumu. Anza kufanya mawasiliano yako kuwa ya wazi kadiri inavyowezekana ili
kuzifanya fikra za mwenzi wako kutowaza tofauti. Ama kama unalazimika
kuongea mambo mengine hasa ya kikazi au kibiashara bila kutakiwa
kusikiwa na mtu yeyote, ni vyema mwenzako akajua hali hiyo mapema ili
kuyaweka mahusianao yako katika hali ya usalama zaidi.
Epuka kuongelea wapenzi wako waliopita
Watu wapendanao huoneana wivu. Hayo ndiyo mapenzi. Si rahisi hata kidogo kwa mtu akupendaye akashindwa kukuonea wivu. Sasa vipi unapoaanza kuzungumzia habari za mahusiano yako yaliyopita
mbele yake? Unataka apate tafsiri ipi? Huo siyo mwanzo wa kumfanya aanze
kuhisi kuwa umemkumbuka zilipedwa wako?
Kwa uhai wa mahusianao yako kitu hiki epuka kabisa. Kwa hali yoyote
jiweke katika mazingira ya kukwepa kuzungumzia mambo yako ya kimahusiano
yaliyopita. Ni hali mbaya inayoweza kufanya mahusiano yako yakaharibika wakati bado unamhitaji mpenzi wako.
Kutozungumzia mahusiano yako ya mwanzo ni moja kati ya mbinu itakayofanya mahusiano yako yaendelee kustawi.
Usijiweke Juu
Ili kuweza kudumisha amani na ustawi wa penzi lako ni lazima usahau
mambo ya kutaka kujiweka juu. Mahusiano yoyote ili yaweze kudumu yapasa
wahusika waheshimiane na kunyenyekeana. Hapo ndipo inapopatikana raha
halisi ya mapenzi.
Raha katika mapenzi haiwezi kupatikana kama mmoja wapo anajiona yuko juu zaidi ya mwengine. Mapenzi hayako hivyo. Mahusiano yote yaliyo katika mtindo huo mwisho wao huwa mfupi mno. Ni
vipi mtu awe na wewe wakati anajiona kama anakubembeleza?
Ni wewe tu
unayetaka kuambiwa unapendwa. Ni wewe tu unayetaka kusikilizwa katika
maamuzi yako. Mapenzi hayo ya wapi? Jiweke katika mazingira bora ya unyenyekevu kwa mpenzi wako uone
matokeo yake. Kila muda atataka kuwa na wewe. Mara zote atataka
kusikiliza sauti yako. Kwa sababu utakuwa burudani yake. Kwa sababu
atakuwa anajua unaiona na kuijali thamani yake.
Kumbuka Binadamu ameumbwa hukosea
Hakuna binadamu aliyekosa mapungufu. Kila bin adamu hukosea. Ni vyema
mpenzi wako anapokukosea kutumia busara na hekima huku ukikumbuka kuwa
kukosea kupo kwa kila bina adamu.
Anayekupenda kwa dhati hawezi akakukosea kwa makusudi. Labda kwa utani. Hivyo unapoona mpenzi kakukosea usijaribu kulitatua hilo tatizo kwa makaripio au maneno ya karaha kana kwamba katenda kosa husika kwa makusudi.
Jitahidi kuwa mpole kadiri utakavyoweza. Mweleze mahali alipokosea. Bila shaka kwa kuwa anakupenda kwa dhati ataona pale alipokosea na kukuomba msamaha. Na ili kudumisha mahusiano yenu unapaswa kumsamehe kwa dhati na maisha kuendelea.
Si vyema hata kidogo kusema kuwa umemshamehe halafu ukawa unalikumbushia tatizo hilo. Kwani hali hiyo itakuwa inamtia unyonge na kupoteza hamu ya kuwa karibu na wewe. Ni nani anapenda kusemwa semwa kama mtoto mdogo? Nani anapenda kusimangwa kwa ajili ya makosa yake yaliyopita? Bila shaka jibu lake ni hakuna. Usiwe mtu wa aina hiyo kwa maendeleo bora ya mapenzi yenu.
Omba msamaha unapokosea
Pindi unapomkosea mpenzi wako ni vyema sana kumuomba msamaha. Ni kitendo cha kuonesaha kujali na kuthamini. Kama tulivyotangulia kuona hapo juu kuwa kukoseana kwa binaadamu huwa kupo, ila kitu cha msingi ni kutambua kosa na kuomba msamaha.
Hakikisha kuwa hurudii tena kosa ulilofanya kwa maana kwa kufanya hivyo itafanya hata siku nyingine unapoomba msamaha aone unatania na humthamini kwa kiwango stahili na ndiyo maana licha ya kukusamehe mara kadhaa lakini huwa huonekani kujifunza kutokana na msamaha anaokupa.
Omba msamaha kwa dhati. Huku akili yako ikiwa makini kutorudia tena kosa. Kuomba msamaha si kitendo cha udhaifu au unyonge kama fikra za wengi zinavyoamini. Ni kitendo cha uungwana na ustaarabu na hufanywa na watu wenye akili timamu na hekima. Omba msamaha unapokosea. Kudhihirisha kuwa kosa husika liltokea kwa bahati mbaya. Mapenzi yako hivyo mpendwa!
Kuwa mkweli
Hii ni ngao ya upendo. Watu wanaopendana huwa wanaambiana ukweli. Ukweli katika mahusiano huyafanya yazidi kushamiri kutokana kila mmoja kuhisi kuthaminiwa na mwenzake. Husababisha kuongeza raha na amani katika mapenzi.
Unapokuwa mkweli kwa mwenzako unafanya hata wanafki wakose pakuanzia. Wataanzia wapi wakati kila kitu unachofanya mpenzi wako anajua? Ukienda sokoni anajua. Ukipitia saluni anajua. Lakini balaa huanza pale unapokua na tabia ya kuongopa.
Maana baada ya mpenzi wako kutaka kujua mahali ulipopitia au kitu ulichofanya na wewe kukana, wanafiki wataanza kumpa ushahidi wa mambo; hawatoishia hapo tu bali wataongeza hata yale yasiyokuwamo. Hapo ndiyo kwenye matata.
Mpenzi wako ataanza kuhisi mambo tofauti japo hukufanya. Hisia zake hizo potofu zinaweza kushibishwa na uongo wako. Atajiuliza kama hukuwa na nia au maana mbaya kwanini unadanganya? Kazi kwako. Jitahidi kuwa mkweli kadiri inavyowezekana katika
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :