KENYA KUPOKEA WAGONJWA 400 WA KANSA KUTOKA UGANDA

No comments
Friday, April 15, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Uganda imetangaza kwamba wagonjwa 400 wanaohitaji matibabu ya kansa watapelekwa Kenya baada ya mashine pekee ya kuwahudumia wagonjwa nchini humo kuharibika. Wagonjwa hao ni kati ya jumla ya wagonjwa 17,000 wanaohitaji huduma ya tibaredio.


Hatua hiyo inatokana na kuharibika kwa mashine ya kutibu saratani (Radiotharapy), katika Hospitali kuu ya Mulago ambapo kwa mujibu wa Msemaji wa idara ya kutibu saratani katika hospitali kuu ya Mulago Hospitali hiyo ilipokea wagonjwa elfu nne mwaka uliopita. Asilimia 75 ya wagonjwa hao walihitaji matibabu ya Radiotherapy. 

Waziri wa afya nchini humo Dkt Chris Baryomunsi aliambia bunge la nchi hiyo Alhamisi kwamba hospitali ya kibinafsi ya Aga Khan jijini Nairobi imejitolea kusaidia wagonjwa 400 kutoka Uganda wanaohitaji matibabu.

Gazeti la kibinafsi la Daily Monitor, likinukuu maafisa wa serikali, linasema nchini Uganda kuna visa 32,000 vya kansa. Asilimia 55 (sawa na wagonjwa 17,600) wanahitaji huduma ya tibaredio. 

Kwa mujibu wa Dkt Baryomunsi, serikali ya Uganda itagharimia usafiri na malazi huku hospitali ya Aga Khan nayo ikigharimia matibabu. Mashine pekee nchini humo ilikuwa katika hospitali kuu ya Mulago ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi ya matibabu nchini Uganda na hushughulikia magonjwa makubwa.

Mashine ya tibaredio iliyokuwa Mulago ambayo ni aina ya Cobalt 60 hutoa miali nururishi, yaani Radioactive, kuangamiza seli za saratani katika mwili wa mgonjwa. Ilinunuliwa mwaka wa 1995 na imekua ikiharibika mara kwa mara, licha ya kukarabatiwa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .