MAOFISA WAKUU 8 WA CHASE BANK NA NBK-KENYA KUKAMATWA
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Kenya ameagiza maafisa wanane wakuu wa benki nchini Kenya wakamatwe. Taarifa
kutoka kwa mkuu huyo Joseph Boinnet imewataka maafisa sita kutoka kwa
Benki ya National na wawili kutoka kwa benki ya Chase wafike kwa polisi
kuandikisha taarifa la sivyo wakamatwe.
Maafisa hao wanatuhumiwa kuhusika katika ukiukaji wa maadili. Benki
ya Chase iliwekwa chini ya mrasimu Alhamisi baada ya shughuli katika
benki hiyo kukwama kutokana na watu kutoa pesa kwa wingi.
Wateja
walianza kuhamisha pesa kutoka kwa benki hiyo baada ya kuenea kwa
wasiwasi kuhusu uthabiti wa benki hiyo kifedha. Habari hizo zilienezwa
sana kupitia mitandao ya kijamii.
Bw Boinnet amesema mwanamume mmoja amekamatwa kwa “kueneza uongo” kwenye mitandao ya kijamii kuhusu sekta ya benki. Amewatahadharisha wananchi dhidi ya kusambaza habari kama hizo.
Benki
Kuu ya Kenya (CBK) imesema wasiwasi uliotokana na kuenezwa kwa habari za
uongozi kuhusu benki ya Chase ndizo zilizopelekea watu wengi kutoa pesa
zao Jumatano na kulemaza benki hiyo.
Gavana wa CBK Dkt Patrick Njoroge amekuwa akikabiliana na maafisa
walio waadilifu katika sekta ya benki nchini Kenya tangu kuchukua
usukani.
"Hatuwezi kuwavumilia maafisa wa benki ambao ni wahuni,
wale wanaoiba kutoka kwa watu wanaoweka akiba pesa zao,” Dkt Njoroge
amenukuliwa na shirika la habari la Reuters. Jumatano, benki ya
Chase ilimsimamisha kazi mwenyekiti wake na meneja mkurugenzi baada ya
kutolewa kwa taarifa mbili kinzani za matokeo ya kifedha.
Moja
ilishusha mikopo iliyochukuliwa na maafisa wa ndani wa benki hiyo.
Nyingine ilionyesha wakurugenzi walikuwa wamekopeshwa $80m, na mikopo
isiyolipwa katika benki hiyo ilikuwa imepanda na kufika $100m.
Mnamo
29 Machi, Benki ya National iliwatuma kwenye likizo ya lazima afisa
mkuu mtendaji na mameneja watano wakuu kupisha ukaguzi wa kifedha katika
benki hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :