REALD MADRID, MAN CITY ZATANGULIA NUSU FAINALI UEFA

Posted in
No comments
Wednesday, April 13, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Timu ya soka ya Real Madrid inayonolewa na gwiji wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane, imefanikiwa kuwaondoa Klabu ya Ujerumani ya Wolfsburg na kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa ulaya (UEFA), kwa ushindi wa jumla wa 3-2.



Alikuwa ni mchezaji nyota na nahodha wa Ureno, Christiano Ronaldo aliyewanyanyua mashabiki wa Madrid huku akiwanyamazisha Wolfsburg ambao walikuwa kifua mbele ya mabao 2-0 kutokana na mechi ya mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Ujerumani, juma moja lililopita.

Kama kawaida yake, Ronaldo alitupia Hat Trick (3-0) na kuwafanya vijana wa Zidane watinge nusu fainali kwa mara ya sita mfululizo (2010/11, 2011/12, 2012/13, 2013/14, 2014/15 na sasa 2015/2016).

Kwingineko Manchester city imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuwafunga Psg ya Ufaransa jumla ya bao 1-0. Wakicheza katika dimba lao la Etihad Manchester city walifanikiwa kuandika bao pekee na la ushindi Dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji De Bruyne.

Kwa ushindi huo Manchester city wameifunga Psg jumla ya mabao 3-2 baada ya timu hizo kufungana bao 2-2 katika mchezo wa awali.

Michuano hii inaendelea tena Jumatano kwa michezo miwili, Benfica itamenyana na Bayern Munich huku Atletico Madrid ikichuana na Barcelona katika dimba la Vicente Calderon.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .