Barcelona yamnasa mchezaji kutoka Colombia

Posted in
No comments
Friday, May 27, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mara baada ya kumaliza vizuri msimu huu kwa kutwaa taji la ligi, La Liga na lile la Copa del Rey, Kocha Luis Enrique wa FC Barcelona ameamua kuimarisha kikosi chake hasa kufuatia matokeo duni kwenye EUFA Champions League kwa kufanya usajili.

Kwa mujibu wa The Mirror, Klabu hiyo iliyopo katika mji wa catalunya imetumia pound milioni 2.8 kumsajili Davinson Sanchez, raia wa Colombia kutoka klabu ya Atletico Nacional ambapo taarifa zaidi zinasema kuwa beki huyo atakuwa mazoezi na  kikosi cha kwanza hiyo ni kwa mujibu wa Kocha Luis Enrique. 


Harakati za vilabu vya Ulaya kuanza kuwania saini za mastaa wanaowahitaji katika msimu wa 2016/2017 zimeshaanza, leo May 27 2016 ambapo pia mbali na FC Barcelona Klabu kama Chelsea, Manchester United na Arsenal ziko mbioni kuimarisha vikosi vyao.




Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .