Injera aweka rekodi mpya ya dunia katika mchezo wa Raga

No comments
Saturday, May 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Ni dhahiri kuwa Mchezaji wa Timu ya taifa ya mchezo wa Raga ya Kenya 7s maarufu kama Shujaa, Collins Injera anaipenda sana na ana bahati na uwanja wa Twickenham. utashangaa ni kwanini, ila ukweli ni kwamba uwanja huu umeshuhudia mwanamichezo huyu akipiga hatua kubwa ya mafanikio katika mchezo huu.
Injera alifunga 'try' yake ya kwanza hapo, akahitimisha mchezo wake wa 50 hapo, alifunga 'try' yake ya 200 mwaka jana kwenye uwanja huu, na sasa ameingia katika vitabu vya kumbukumbu vya mchezo huu unaopendwa sana nchini Kenya ukiacha Soka na Riadha, baada ya kufanikiwa kuvunja rekodi ya kufunga 'try' 230, iliyowekwa na Kocha wa Argentina Santiago Gomes Cora miaka kadhaa iliyopita.
Nahodha huyo msaidizi wa Shujaa sasa anashikilia rekodi ya kufunga 'try' nyingi zaidi baada ya kufunga 'try' 231 kwenye HSBC World Rugby Series, katika mchezo mkali uliopigwa siku ya jumamosi (May 21, 2016) dhidi ya Scotland ikiwa ni katika mashindano ya England 7s.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .