Manchester United Yatwaa Kombe la FA

Posted in
No comments
Saturday, May 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Manchester United inayonolewa na Mdachi anayekalia kuti kavu, Luis Van Gaal, aimefanikiwa kutwaa kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004. Man United imefanikiwa kutwaa kombe hilo katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa muda mfupi uliopita katika dimba la Wembley dhidi ya Cristal Palace na kuibuka na ushindi wa 2-1.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata kunako Dakika ya 81 ya kipindi cha pili huku la ushindi likipata katika akika 110 kupitia kwa mchezaji kinda Jesse Lingard. Cristal Palce ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 78, kupitia kwa Jason Puncheon.
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofanya vizuri tangu achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo akimpokea Kocha mwenye heshima, Sir Alex Gurguson. Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Kikosi cha Man Utd: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Fellaini, Mata, Rooney, Martial, Rashford

Kikosi cha Palace: Hennessey; Ward, Dann, Delaney, Souare; Zaha, Cabaye, McArthur, Jedinak, Bolasie; Wickham.
Uwanja: Wembley

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .