Jux: hivi ndivyo nilivyomnasa Vanessa Mdee

Posted in
No comments
Saturday, May 21, 2016 By danielmjema.blogspot.com


Msanii Jux amefunguka na kusimulia namna alivyoweza kumnasa na kumuweka kwenye imaya yake ya mapenzi Vanessa Mdee na kusema kuwa kwa mara ya kwanza aliweza kuonana kwa mara ya kwanza na Vanessa Mdee studio na hapo ndipo walipoanza kujenga taratibu mahusiano yao.
Kupitia kipindi cha Mkasi Jux amesema kuwa yeye lengo lake kubwa lilikuwa ni kufanya wimbo ambao alipenda kumshirikisha msanii wa kike anayeweza rap hivyo Pancho Latino alimsikilizisha kazi za Vanessa Mdee na akamkubali na kuamua kufanya naye kazi.
“Mara ya kwanza nimekutana na Vanessa Mdee Studio kwa Pancho Latino nilienda kufanya kazi pale na nikawa nahitaji msichana ambaye ni mzuri kwenye kurap ili nimshirikishe hivyo basi Pancho akaniambia kuna msichana yupo mzuri, akanisikilizisha kazi zake nikazipenda japo niliona kama mzungu sana na kumwambia Pancho huyu tutambadilisha kidogo, hivyo kesho yake nilipoenda studio nikakutana na Vanessa pale tukafanya kazi tulipomaliza ilibidi nimrudishe kwao kwani kipindi hicho alikuwa hana usafiri”. Alisema Jux
Jux aliendelea kusimulia na kusema kuwa walikuja kukutana siku nyingine kwenye show ambapo wote walialikwa na siku hiyo ndipo alipata nafasi ya kumuangalia vizuri na kugundua kuwa Vanessa ni mtu wa aina yake.
“Siku ya pili tulikutana naye kwenye show baada ya ngoma zake kutoka na kusikika mtaani, siku hiyo nilimwangalia hivi Vanessa nikawa sijielewi elewi ila nilipata nafasi ya kuongea naye kwa muda mfupi sana ila maongezi yale yalikuwa na maana sana, sasa kulikuwa na kidude fulani cha kijani mkononi alikuwa amekivaa nikakiomba akaniambia Jux this is very special siwezi kukupa bhana. Lakini kesho yake aliniita niende kuchukua kile kidude lakini mambo yangu yakawa mengi nikashindwa kwenda, hivyo kile kidude ndiyo kilikuwa chanzo cha mimi na Vanessa kukutana wawili” alisimulia Jux
eatv.tv

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .