Mifuko ya Plastiki marufuku kutumika nchini Tanzania kuanzia 2017
Posted in
afrika mashariki
No comments
Sunday, May 29, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, imetangaza kupiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.
Akitoa agilo hilo, Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, January Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.
Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
>>>‘Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’
>>>’tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘
Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.
Habari Zingine
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :