Love Talk: Kama Bado uko Single, Fanya haya kabla ya kuingia katika Mahusiano
Posted in
Maisha
No comments
Sunday, May 29, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mahaba niue, Mapenzi yanaumiza sana, na kabla hujaanza kuwaza kumtokea msichana mwingine au wewe dada kumkubali yule mshikaji alikuwa anakufwatilia kwa mwaka sasa, fanya haya yafuatayo:
Jipende kupita maelezo
Tumia muda huu ambao uko single na ujipende zaidi kuliko ulivyokuwa katika mahusiano, muda wa kujiwaza wewe, kula vizuri, vaa vizuri, pata muda mwingi wa kupumzika, tembelea sehemu za starehe mwenyewe bila kuwaza kutafuta mtu mwingine na utajifunza kitu.
Kuna na Marafiki wa jinsia tofauti na wewe
Jichanganye na marafiki wa jinsia tofauti na wewe na ujifunze mambo ya mahusiano kupitia kwao, toka nao matembezini au sehemu za michezo ila usianze mahusiano mapema kama hauko tayari.
Kuwa Karibu na Ndugu zako
Huwezi jua ni kwa kiasi gani umekaa mbali na watu wako wa karibu wakati ukiwa uko busy na mpenzi wako. Wakati kama huu utumie kutoka na ndugu zako wa karibu au kushinda nyumbani mwisho wa wiki, pamoja na familia yako.
Fanikisha Ndoto zako
Ukiwa katika mahusiano kila kitu lazima kiwe kwa ajili ya wote wawili ila kama upo single ni raisi kufanya kitu kwa ajili yako mwenye na tumia muda huu kufanikisha ndoto zako, fikiria malengo yako zaidi ili ufanikiwe.
Jiulize unataka nini kwenye Mahusiano
Tumia huu muda, kuangalia ni aina gani ya mpenzi unamuhitaji na nini kitakupa furaha kutoka kwake, ila pia tambua furaha kama haipo kwako huwezi tegemea kuipata kwa binadamu mwingine. Kwahiyo jua ni jinsi gani utakuwa na furaha bila kutegemea mapenzi au kuwa na mpenzi.
Fanya kitu kipya
Kama kufuga mbwa ,paka au chochote ambacho hujawahi fanya hakikisha haukosi cha kufanya ili usiwe mpweke, Tembelea mbuga za wanyama au nenda nchi nyingine kama una uwezo na jifunze vitu vipya.
Jenga ukaribu na Marafiki zako
Inasemekana kuwa marafiki wengi hupoteana au huwa hawana tena mazoea ya karibu pindi wanapoanza mahusiano, angalia umeshakuwa mbali na marafiki zako wangapi toka uanze mahusiano na jenga tena urafiki na watu wako.
Zingatia kusubiri kabla hujaanza mahusiano mapya, unaweza kujiingiza kwenye mahusiano mengine ambayo yatakuwa matatizo kuliko ulipotoka na ukajikuta unajutia maamuzi yako.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :