Showing posts with label Maisha. Show all posts
Showing posts with label Maisha. Show all posts

Hapa ndipo atakapoishi Obama baada ya kutoka White House

Hapa ndipo atakapoishi Obama baada ya kutoka White House

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wakati Taifa la Marekani likikaribia kuingia katika Uchaguzi utakaohitimisha utawala wa Rais Barack Obama, aliyeingia madarakani mwaka 2008, ni wengi wanatamani kufahamu ni wapi Rais huyo atakapoishi baada ya White House.
July 2 2016 CCN wameonesha video ya nyumba atakayoishi Rais Obama baada ya kukabidhi madaraka January 2017 na kuondoka White House.
Kupitia kituo kikubwa cha TV Marekani na Dunia nzima Rais Obama baada ya kustaafu ataendelea kuishi Washington na atakuwa akiishi katika nyumba yenye vyumba 9, nyumba ambayo inatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 6.3 ambazo ni zaidi ya Ksh Bilioni 5.652.

Mama akubaliwa kubeba mimba ya mwanae

Mama akubaliwa kubeba mimba ya mwanae

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mwanamke ambaye anataka kutumia mayai ya uzazi ya bintinye ili kumzaa mjukuu wake ameshinda kesi mahakanani na kuruhusiwa kufanya hivyo.


Mwanamke huyo wa umri wa miaka 60 alikuwa amekatazwa kupeleka mayai ya bintiye kwenye kliniki moja nchini Marekani hali iliyosababisha akate rufaa.
Bintiye ambaye aliaga dunia mwaka 2011, anaripotiwa kumuambia mamake amzalie watoto wake. Lakini mamake alishindwa katika kesi mwaka uliopita.
Hata hiyo aliruhusiwa kupinga hukumu hiyo katika mahakama ya rufaa mjini London mbele ya jopo la majaji watatu.
Mwaka 2014 halmashauri inayohusika na mayai ya uzazi, ilisema kuwa mayai hayo hayangetolewa mjini London, kwa sababu bintiye hakuwa ametoa idhini kamili kabla ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini kwenye kesi ya sasa mawakili waliawaambia majaji kuwa, mwanamke huyo alikuwa anataka kutimiza matakwa ya bintiye ya kuzaa mtoto akitumia mayai yake na kisha amlee mtoto huyo.
Source:BBC

Love Talk: Kama Bado uko Single, Fanya haya kabla ya kuingia katika Mahusiano

Love Talk: Kama Bado uko Single, Fanya haya kabla ya kuingia katika Mahusiano

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mahaba niue, Mapenzi yanaumiza sana, na kabla hujaanza kuwaza kumtokea msichana mwingine au wewe dada kumkubali yule mshikaji alikuwa anakufwatilia kwa mwaka sasa, fanya haya yafuatayo:

Jipende kupita maelezo



Tumia muda huu ambao uko single na ujipende  zaidi kuliko ulivyokuwa katika mahusiano, muda wa kujiwaza wewe, kula vizuri, vaa vizuri, pata muda mwingi wa kupumzika, tembelea sehemu za starehe mwenyewe bila kuwaza kutafuta mtu mwingine na utajifunza kitu.
Kuna na Marafiki wa jinsia tofauti na wewe
Jichanganye na marafiki wa jinsia tofauti na wewe na ujifunze mambo ya mahusiano kupitia kwao, toka nao matembezini au sehemu za michezo ila usianze mahusiano mapema  kama hauko tayari.
Kuwa Karibu na Ndugu zako
Huwezi jua ni kwa kiasi gani umekaa mbali na watu wako wa karibu wakati ukiwa uko busy na mpenzi wako. Wakati kama huu utumie kutoka na ndugu zako wa karibu au kushinda nyumbani mwisho wa wiki, pamoja na familia yako.
Fanikisha Ndoto zako
Ukiwa katika mahusiano kila kitu lazima kiwe kwa ajili ya wote wawili ila kama upo single ni raisi kufanya kitu kwa ajili yako mwenye na tumia muda huu kufanikisha ndoto zako, fikiria malengo yako zaidi ili ufanikiwe.
Jiulize unataka nini kwenye Mahusiano
Tumia huu muda, kuangalia ni aina gani ya mpenzi unamuhitaji na nini kitakupa furaha kutoka kwake, ila pia tambua furaha kama haipo kwako huwezi tegemea kuipata kwa binadamu mwingine. Kwahiyo jua ni jinsi gani utakuwa na furaha  bila kutegemea mapenzi au kuwa na mpenzi.
Fanya kitu kipya
Kama kufuga mbwa ,paka au chochote ambacho hujawahi fanya hakikisha haukosi cha kufanya ili usiwe mpweke, Tembelea mbuga za wanyama au nenda nchi nyingine kama una uwezo na jifunze vitu vipya.
Jenga ukaribu na Marafiki zako
Inasemekana kuwa marafiki wengi hupoteana au huwa hawana tena mazoea ya karibu pindi wanapoanza mahusiano, angalia umeshakuwa mbali na marafiki zako wangapi toka uanze mahusiano na jenga tena urafiki na watu wako.
Zingatia kusubiri kabla hujaanza mahusiano mapya, unaweza kujiingiza kwenye mahusiano mengine ambayo yatakuwa matatizo kuliko ulipotoka na ukajikuta unajutia maamuzi yako.

Shukurani toka kwa Familia ya Issa Michuzi kufuatia msiba wa mwanae Maggid

Shukurani toka kwa Familia ya Issa Michuzi kufuatia msiba wa mwanae Maggid

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.

Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.

Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue  pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa  kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa.

TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi  wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. 

MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote.  ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani  za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.

Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba  mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na  Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. 

TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA  KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...

Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!

CHOKORAA WASAKA MAISHA KENYA

CHOKORAA WASAKA MAISHA KENYA

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Nchini Kenya kunaongezeko la tatizo la watoto wa mitaani, ambao wanakataliwa na jamii hatua inayowasukuma kutafuta namna ya kuishi. Wakati hayo yanatokea, serikali haina mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo.



Shirika la kimataifa linaloshughulika na ustawi na haki za watoto wa mitaani, CSC, inasema idadi ya watoto waishio mitaani nchini Kenya, inaweza kuwa kati ya 250,000 na 300,000, wakiwemo 60,000 ambao wako jijini Nairobi pekee.

Katika kitongoji cha Mlango Kubwa, katikati mwa jiji la Nairobi, sehemu lililopokuwa jalala hapo zamani ni kimbilio la watoto wa mitaani, ambapo wanapaita kama makao makuu. Kwa mujibu wa shirika hilo, katika eneo hilo watoto wanalala kwenye sakafu ngumu, karibu kabisa na eneo zinapotupwa takataka, ambako huokoteza mabaki ya takataka na kuyauza ili kupata fedha.

Watu huwaona watoto hawa kama si binadamu, anasema Moha, ambaye pia aliwahi kuwa mtoto wa mtaani, lakini hatimaye alifanikiwa kuyaacha maisha hayo magumu, na sasa ni mchezaji kwenye bendi za dansi. Anasema, watu wakiwaona wananusa gundi na wakiwa wachafu huwapiga na kuwatukana.

Baadhi yao hujiingiza kwenye maisha hayo baada ya kufiwa na wazazi wao, labda kutokana na ugonjwa wa Ukimwi na wengine hukimbia unyanyasaji majumbani kwao. Lakini wengine wanaishi mitaani kwa sababu tu familia zao zinaishi katika hali ya umaskini na haziwezi kuwalea.

Moha anasema kuwa ni vigumu kuileezea hali wanayokumbana nayo, kwani unaweza kukuta kama wamelala nje ya duka la mtu, asubuhi mwenye duka badala ya kuwaamsha taratibu, huwapiga mateke au kuwamwagia maji.

Wakiwa wametelekezwa na serikali, baadhi ya taasisi za kibinadamu huwasaidia. Alfajiri ni miongoni mwa taasisi hizo, na ni mradi uliobuniwa na msanii kutoka nchini Australia Lenore Boyd, anayewafundisha watoto hao sanaa ya uchoraji.

"Kila mmoja anapaswa kufikiria namna watoto hawa wanavyochukuliwa, na ni kwa nini wanaishi mitaani na mateso wanayokutana nayo huko mitaani'', amesema Boyd. Watoto hawa wameathirika kimaisha, ni watoto waliopitia mateso makubwa, wametelekezwa. Kwenda mitaani ni hatua ya kukata tamaa.

Wasichana ndio hukutana na wakati mgumu zaidi. Kituo cha kuwasaidia wasichana wanaoishi mitaani, The Rescue Dada, kilichopo Nairobi, kwa zaidi ya miongo miwili kimekuwa kikiwasaidia wasichana hao kwa kuwawezesha kurudi kwenye maisha yao ya kawaida. Kituo hicho kilicho na mabweni mawili na madarasa, kina wasichana 70 na kinatoa msaada wa kisaikolojia na elimu, na kuwezesha juhudi za kuwaunganisha tena na familia zao.

"Maisha ya mjini ni magumu sana. Mtu kulala nje, kwenye baridi na mara nyingine unanyeshewa mvua. Kuna wakati unaweza kuamka asubuhi na kukuta mwenzenu amekufa," anasema Janet, msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyejiunga na kituo hicho hivi karibuni. Janet anasema wengine huishia kuuza miili yao ili kupata fedha za kununua chakula.

Miongoni mwa wasichana walioandikishwa kituoni hapo mwaka 2014, karibu theluthi yao walipitia unyanyasaji wa kingono, na wengine walibakwa na kundi la wanaume. Wengi wao walilazimishwa kuuza miili yao, huku kukiwa na hatari kubwa ya kupata Ukimwi.

Mkurugenzi wa kituo hicho Mary Njeri Gatitu, anasema kuwasaidia kurudi katika maisha yao ya kawaida kutachukua muda mrefu, ingawa anafanya kila linalowezekana kusaidia kile anachoamini anaweza kukifanya. Anasema ni sawa na tone la maji kudondokea katika bahari, kwa sababu serikali haijalishughulikia vya kutosha suala la umasikini nchini Kenya.

NJOO TUSHEHEREKEE MEI MOSI PAMOJA NA SKYLIGHT BAND LEO NDANI YA KIOTA CHATHAI VILLAGE, MASAK

NJOO TUSHEHEREKEE MEI MOSI PAMOJA NA SKYLIGHT BAND LEO NDANI YA KIOTA CHATHAI VILLAGE, MASAK

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower(wa kwanza kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku msanii mwenzake Sony Masamba akiendlea kuzirundi ngoma ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Usikose leo kwenye shoo yao maana kuna vitu vingi vipya.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi uku wakisindindikizwa na dada mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Ashura Kitenge(wa kwanza kushoto).
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakiziruzi ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower(wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Burudani ikiendelea.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower(wa kwanza kushoto) akiongoza kikosi cha bend ya Skylight waliokuwa wakitoa burudani kwa mashabiki wao (hawapo picha) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
Waimbaji wa Skylight Band wakicheza moja ya nyimbo zao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo(hawapo pichani) waliofika kwenye Kiota Cha Thai Village kuburusika na Bendi hiyo.
Msanii wa bendi ya Skylight, Sony Masamba akicheza mmoja ya style mpya ya bendi hiyo mbele ya mashabiki wao(hawapo pichani)
Joniko Flower na Sony Masamba wakiwatizama mashabiki wa bendi hiyo kama wamejua kucheza style mpya.
Msanii wa Bendi ya Skylight, Sony Masamba(wa kwanza kushoto) akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Ashura Kitenge(wa kanza kulia) pamoja na Sam mapenzi( katikati)
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani)
Mashabiki wakiendelea kuziruka ngoma za bendi ya Skylight
Waimbaji wa bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar usikose leo njoo na yule umpendae ili ujionee raha ya bendi hii
Mambo ya Selfie hayakosi ndani ya Kiota cha Thai village wakati wa beni ya Skylight ikiendelea kutoa burudani.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower (wa kwanza kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Sony Masamba (katikati) pamoja na Sam mapenzi (wa kwanza kutoka kulia)
Mashabiki na wapenzi wa Bendi ya Skylight wacheza mduara wakati wa bend hiyo ikitoa burudani ndani ta kiota cha Thai Village masaki jijini Dar.
Ashura Kitenge akiimba mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na wanamziki wenzake ambao ni Sony Masamba(wa kwanza kushoto), Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47(wa pili kutoka kushoto) pamoja na Joniko Flower(wa kwanza kutoka kulia)
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower(wa kwanza kushoto) akiimba na mwanamziki mwenzake Sony Masamba ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Joniko Flower na mwanamziki mwenzake Sony Masamba wakizirudi ngoma za kikongo
Ashura Kitenge akiimba mbele ya mashabiki wa Skylight Band(hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47(kushoto) pamoja na Sam Mapenzi(kulia)
Ilikuwa ni kusakata rumba mpaka kuchwee yaani ilikuwa ni noma sana
Mmoja wa mashabiki wa Bendi ya Skylight akichukua kumbukumbu

Baada ya Kajala kudai Wema ni mnafiki,Wema aamua kujibu mapigo. 'Amlipua' vibaya Kajala

Baada ya Kajala kudai Wema ni mnafiki,Wema aamua kujibu mapigo. 'Amlipua' vibaya Kajala

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji  Kajala kudai kuwa mrembo Wema Sepeteu ni Mnafiki, hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari  ambayo  ilisambaa  katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii.
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? 

Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK

Gwajima afunguka sakata la Mbasha

Gwajima afunguka sakata la Mbasha

No comments
By danielmjema.blogspot.com
gwajima na mbasha
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima (kushoto) na Emmanuel Mbasha (kulia), mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha.
MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima, amefunguka na kuuweka hadharani uhusiano wake na familia ya waimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha na mume wake, Emmanuel Mbasha.
Gwajima amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Flora na kwamba hatua hiyo inadaiwa kuchangia mvurugano kwenye ndoa ya wanamuziki hao.
Mbali ya kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Flora, pia anatajwa kuwa nyuma ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambapo kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha mchungaji huyo na kesi hiyo iliyoanza kutajwa Juni 17 mwaka huu.
Akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu sakata hilo kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili, Gwajima akiwa katikati ya madhabahu ya kanisa lake lililopo Kawe jijini Dar es Salaam huku akiwa na wasaidizi wake pamoja na watoto wake wawili, alisema taarifa zinazoenezwa ni za kijinga na hazina ukweli wowote.
Alisema mgogoro wa Mbasha na Flora unaonekana kuwa ni wa muda mrefu na kwamba umekuja kujitokeza kanisani kwake baada ya kuanza kufanya nao kazi ya kutoa huduma ambapo wawili hao walikuwa waburudishaji kwenye mikutano yake.
“Nilimfahamu Flora na Mbasha mwezi wa tisa mwaka jana… kipindi hicho nilikuwa na mkutano Arusha. Wote wawili niliwaalika tukaenda nao kwenye mkutano na pindi mkutano ulipomalizika walirudi nyumbani tukaenda tena katika mikoa mingine ya Moshi, Tanga, Morogoro na Kilombero wote wawili walikuja kushiriki mikutano hii kama waimbaji na wote walirudi nyumbani kwao.
“Nimekuwa nikiona kwenye mitandao wakisema kuwa nilikwenda na Flora peke yake katika baadhi ya maeneo kama Morogoro… si kweli, muda wote walikwenda wote wawili na walirudi wote wawili, pia sina uhusiano wa kimapenzi na Flora kama inavyodaiwa.
“Kwanza watu wote waliokwenda kwenye mkutano walikuwa 300, kila mkoa walikuwa watu 300. Naamini kuna mtu ana hoja zake binafsi anataka kuudanganya umma kwamba Gwajima ana uhusiano na Flora.
“Nataka niwakumbushe Watanzania kuwa baada ya kumaliza hii mikutano hawakuwa washirika wetu kanisani, kwa maana kuwa hawakuwa wakisali kanisani kwangu kwa sababu tuliwaalika kuja kuimba na walikuwa wanalipwa kwa sababu ya kuimba pekee,” alisema.
Aidha alisema baada ya kumaliza mikutano hiyo na kukaa kwa muda, Flora aliamua kwa mapenzi yake kwenda kusali kanisani kwake na baadaye mumewe naye akajiunga na mke wake kushiriki ibada kwenye kanisa lake.
Akizungumzia suala la kuwa nyuma ya kesi inayomkabili Mbasha na kuwa amekuwa akimpatia fedha Flora ili kufanikisha dhamira ovu dhidi ya mumewe, Gwajima alisema si la kweli.
“Hili suala la kumpatia fedha Flora ili amuangamize mume wake halina ukweli, ukweli ni kwamba baada ya Mbasha kutuhumiwa kubaka alitoweka nyumbani, mke wake hakuwa na sehemu ya kupata msaada, kutokana na hali hiyo ndipo Flora alikuja kanisani kwetu kuomba msaada wa fedha na kwa vile ni mshirika wetu tulimsaidia.
“Nilizungumza na wachungaji wenzangu tukaona ni vyema tuitishe harambee ili waumini wamchangie kama wanavyochangia watu wengine wenye matatizo mbalimbali kwa sababu Flora alisema jamani hana fedha na mume wake amemkimbia na hana chochote, watu wakamchangai!
“Sasa nadhani zipo fikra kwamba, Gwajima anachangisha fedha za Flora ili apate fedha za kuendelea kumshtaki mumewe, pia zipo fikra kwamba kanisa langu ndilo limemzuia Flora kurudi kwake.
“Zikianza kusambazwa picha mbaya za Gwajima kwenye mitandao ya kijamii ili nichukue uamuzi wa kumfukuza Flora kanisani kwangu ili akapate matatizo, siwezi kumfukuza Flora kanisani kwangu wala hilo halitatokea… nimechukua hatua mbalimbali ikiwamo kumshauri Flora arudi kwa mume wake lakini alikataa mwenyewe,” alisema.
Aidha, Mchungaji huyo pamoja na kukanusha kuwa yeye sio chanzo cha mgogoro huo pia alisema hajamsomesha wala hakuwahi kutoa fedha za kufadhili masomo ya Flora nchini Uingereza.
“Unaweza kumpeleka ng’ombe kisimani lakini jukumu la kunywa maji ni lake, akikataa ni mwenyewe, akinywa ni mwenyewe, mimi siku zote nawashauri Flora na Mbasha wawe na uhusiano mzuri, warudishe uhusiano wapatane, hata kesho (leo) nitampigia simu baba yake mzazi Mbasha na wadogo zake ili nijaribu kuwaita tena kujaribu kuona kama tunaweza kuwasaida kuwarejesha kwenye ndoa yao.
“Hata hivyo uamuzi wa kurudiana bado utakuwa ni wa kwao wao mimi siwezi kuwalazimisha,” alisema.
Mbasha (32) alipandishwa kizimbani Juni 17 mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Wilberforce Luago.
Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai mshtakiwa ambaye pia ni mfanyabiashara alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam.
Kesi ya Mbasha inatarajia kusomwa tena Juni 17, mwaka huu kwenye Mahakama hiyo ambapo mshtakiwa huyo yuko nje kwa dhamana.

HATIMAYE MALKIA NA RAIS MPYA WA KIJIJI CHA MAISHA PLUS WAPATIKANA

HATIMAYE MALKIA NA RAIS MPYA WA KIJIJI CHA MAISHA PLUS WAPATIKANA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Malkia Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Elizabeth Masha kutoka Morogoro Tanzania 
Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati ya hao mmoja hupatikana na  Marais  waliopita hawapatiwi nafasi ya kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa Malkia wa Kijiji hicho.
 
Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha kutoka Nchini Kenya

Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapo idadi ya washiriki 36 wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus  ambaye husimamia shughuli zote zinazofanyika katika kijji hicho. 
Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena. 
Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
 Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho. 

Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya. Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja. 
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.

Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.

HONGERENI CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG NA DADA ESTER ULAYA KWA KUUAGA UKAPERA

HONGERENI CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG NA DADA ESTER ULAYA KWA KUUAGA UKAPERA

No comments
By danielmjema.blogspot.com

 Cathbert Kajuna na dada Ester Ulaya hatimaye wamefunga pingu za maisha. Maharusi wote  Mungu awape neema na baraka katika maisha yenu ya ndoa.
Hapa wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.
Kajuna najua hapa presha ilikuwa inapanda na kushuka. Hongera sana kaka.
picha kwa hisani ya anko mo vijimambo blog

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .