Baada ya Kajala kudai Wema ni mnafiki,Wema aamua kujibu mapigo. 'Amlipua' vibaya Kajala
No comments
Saturday, July 19, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji Kajala kudai kuwa mrembo Wema Sepeteu ni Mnafiki, hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari ambayo ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake?
Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK
Habari Zingine
- jaydee: hii ndio siri ya kufanya vizuri miaka yote
- Maskini Mr. Nice azushiwa kifo kwenye Social Media
- Jionee jinsi Kuwait walivyoanikiwa kuivuta bahari nchi kavu ili kutengeneza mji mpya
- SALAMU YA DIAMOND KWA WASANII KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU......NI SHEEEEDAH
- MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA
- MTEMVU ATOA MKONO WA IDD WA VYOMBO NA SH. 10,000 KWA VIONGOZI 912 WA MATAWI YA CCM TEMEKE
- MSANII WA BONGO MOVIE ESTER KIAMA AFUTURISHA WASANII WENZAKE JIJINI DAR
- Baada ya Kajala kudai Wema ni mnafiki,Wema aamua kujibu mapigo. 'Amlipua' vibaya Kajala
- Hapa ndipo atakapoishi Obama baada ya kutoka White House
- Mama akubaliwa kubeba mimba ya mwanae
- Love Talk: Kama Bado uko Single, Fanya haya kabla ya kuingia katika Mahusiano
- Shukurani toka kwa Familia ya Issa Michuzi kufuatia msiba wa mwanae Maggid
- CHOKORAA WASAKA MAISHA KENYA
- Guzo mitandaoni: Thamani ya Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela
- Wasiwasi DR Congo muhula wa Kabila ukifikia kikomo
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :