Spika wa Mombasa akamatwa na Polisi katika Maandamano
Posted in
Breaking News
No comments
Monday, May 23, 2016
By
danielmjema.blogspot.com

Kabla ya kukamatwa kwao kulitokea purukushani kati ya waandamaji na Polisi huku kukiwa na taarifa za awali kuwa zoezi hilo lingefanyika bila kuwepo kwa aina yoyote ya ghasia.
Mamia ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Uhuru Gardens mjini Mombasa kuanzia majira ya saa 1:00 asubuhi tayari kwa ajili ya maandamano ya kuishinikiza Serikali kuridhia kuivunjilia mbali IEBC au kulazimisha maafisa wa tume hiyo kujiuzulu. Polisi nao walikuwa chonjo kukabiliana na matukio yoyote ya uvunjifu wa amani.
Hata hivyo, Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho, Wabunge Abdulswamad Shariff Nassir (Mvita), William Kamoti (Rabai) na Rashid Bedzimba (Kisauni), walifanikiwa kuongoza kile kilichoonekana kuwa ni maandamano ya amani kutoka Bustani ya Uhuru (Uhuru Gardens) kuelekea hadi kwenye ofisi za IEBC zilizoko maeneo ya , Barabara ya Nkurumah (Nkurumah Road).
Citizen tv
Habari Zingine
- Muungano wa Upinzani Kenya (CORD) wanaandamana kuipinga IEBC
- Wetangula awatuhumu Wabunge wa Jubilee kupanga kuvuruga maandamano ya Leo
- MAREKANI: TRUMP ASHINDA NEVADA
- Rais Kenyatta azindua mpango wa kuunganisha Stima katika Nyumba 18,290 Vijijini, ifikapo Juni
- Spika wa Mombasa akamatwa na Polisi katika Maandamano
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :