Dalili nyingine ya Zlatan Ibrahimovic kuelekea kujiunga na Man United

Posted in
No comments
Saturday, June 11, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Usiku wa June 9 taarifa za staa wa zamani wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovich, kuhusishwa kujiunga na klabu ya Man United zimechukua sura mpya ambapo nyota huyo wa Sweden, anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya kujiunga na klabu ya Manchester United.
Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Man United zinazidi kudhihirika, baada ya kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi katika jiji la Manchester ambapo ndio makao makuu au mji inapotoka klabu yaMan United.
bgv
Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika websites ya Proto Group Ltd ambao ni mawakala wa nyumba inaashiria kuwa mipango ya Zlatan kutangazwa kujiunga na Man United ipo tayari kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi, kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris Ufaransa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .