Hotuba ya Rais Uhuru na Raila zatekwa na IEBC

No comments
Wednesday, June 1, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mjadala kuhusu mustakabali wa Tume huru ya uchaguzi nchini (IEBC), iliteka hotuba ya Rais Kenyatta na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga katika hafla mbili tofauti za kuadhimisha miaka 53 ya madaraka (Madaraka Day) ambapo pande zote ziliendelea kushikilia misimamo yao.
Wakati viongzi wa CORD, Raila Odinga na Moses Wetangula wakiendelea kusisitiza kwamba kamwe hawatokubali kushiriki utaratibu wowote wa Kibunge wa kutatua tatizo hilo, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto wamenukuliwa wakiwatuhumu viongozi wa Upinzani kujaribu kukwepa utaratibu uliowekwa kisheria wa kushughulikia swala la IEBC, ambayo ni kupitia Bunge.
Wakenya wengi walikuwa wanatazamia kuwa kikao cha jana (Jumanne) kilichofanyika Ikulu kati ya)  Raila na Wetangula (CORD) na Rais Kenyatta na Ruto (Jubilee), ingeweza kuleta mwafaka. Hata hivyo katika Hotuba zao, Rais Kenyatta na Raila kwa pamoja walikiri kukutana kuhusu swala hilo japo undani wa kilichojadiliwa kikisalia kuwa siri.
Akizungumza mjini Nakuru, katika maadhimisho ya kitaifa ya sherehe za Madaraka Day, Rais Kenyatta alisema alitumia kikao cha Ikulu kumualika Raila na wenzake katika maadhimisho ya Madaraka mjini Nakuru lakini anashangaa imekuwaje viongozi hao wamegoma kuungana na Wakenya na badala wameamua kufanya mkutano wao Uhuru Park.
Akijibu madai ya Rais Kenyatta, Raila ambaye alikuwa Uhuru Park, Jijini Nairobi, alinukuliwa akisema kwamba, walikuwa wameshamuambia kuwa hawatohudhuria sherehe za Afraha kwa sababu mualiko ulikuwa umechelewa na kwamba maandalizi yote ya mkutano wa Uhuru Park yalikuwa yameshakamilika siku nyingi.
For More Visit: citizentv.co.ke

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .