Mahojiano na Makala Jasper kuhusu Tuzo ya National Geographic Society for Leadership
Posted in
afrika mashariki
No comments
Tuesday, June 21, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Makala Jasper ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI). Juni 16, 2016, alitunukiwa tuzo ya National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, akiwa ni mshindi miongoni ma washiriki 30 kutoka barani Afrika.
Tuzo hiyo imetokana na kazi anayofanya pamoja na wananchi katika Vijiji mbalimbali mkoani Lindi.
MCDI huwezesha wanakijiji kutumia rasilimali za misitu kujenga uchumi na kutunza mazingira.
Katika miradi inayofanyika chini ya MCDI, wananchi wameweza kujiendeleza na kujenga shule, hospitali, kununua chakula cha dharura na kutoa misaada kwa vijiji vingine.
Tuzo ya National Geographic Society/Buffet Award ni ya pili kupokelewa na Bw. Jasper.
Ya kwanza ilikuwa Whitley Fund for Nature Award aliyopokea nchini Uingiereza tarehe 27 Aprili, 2016. Karibu umsikilize
Habari Zingine
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :