Rais Kenyatta na Raila waafikiana kuhusu IEBC,
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, June 1, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
VIONGOZI wa Muungano wa Jubilee, iliyoko madarakani na ule wa Upinzani, CORD, jana Jumanne walikubaliana kuanza kwa mazungumzo kuhusu tume huru ya uchaguzi (IEBC), ikiwa ni moja ya njia za kuondoa mvutano ulioko kati ya Serikali na Upinzani nchini.
Wakati ambapo Wabunge kutoka pande zote mbili, wakitafakari namna nzuri ya kurekebisha muundo wa IEBC, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliwakaribisha viongozi wa CORD, Raila Odinga na Moses Wetangula Ikulu Jijini Nairobi kujadili namna ya kuondoa mvutano huo. Kalonzo Musyoka hakuudhuria kwa sababu yuko nje ya nchi.
Raila ambaye alikuwa mjini Narok kuhudhuria mazishi, alilazimika kuvunja ziara yake hiyo na kurejea Nairobi kwa ajili ya kuhudhuria mwaliko huo wa Rais Uhuru Kenyatta. Katika kikao hicho, Rais Kenyatta aliwalika Raila na wenzake kuungana katika sherehe za kitaifa za Madaraka zitakazofanyika mjini Nakuru katika uwanja wa Afraha lakini kwa mujibu wa taarifa tulizozipokea ni kwamba viongozi wamepanga kufanya sherehe hizo Uhuru Park.
Chanzo vyetu kutoka ndani ya kikao hicho cha jana vinasema kuwa, Rais Kenyatta na Raila walikubaliana kuunda jopo la watu 10-watano kutoka kila upande-ambao watakuwa na jukumu la kujadiliana kuhusu njia nzuri ya kuisuka upya tume ya IEBC. Jopo hilo linaanza kukutana kesho (Alhamisi).
Viongozi hao walikutana baada ya kikao cha heshima kilichoandaliwa kwa ajili ya kukutana na Rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye, aliyetembelea Kenya.
“Kila upande litakuwa na jukumu la kuteua wajumbe watano, wanaotokanana bna baraza la maseneta na wabunge wa bunge la taifa, kwa ajili ya kuanza mazungumzo, Jopo hilo litaunda mpango kazi ambao utatumika kutatua malalamiko ambayo CORD wameyatoa kuhusu makamishna wa IEBC,” Kilisema chanzo chetu.
Akizungumza baada ya mazungumzo hayo, Moses Wetangula alisema: “Tumekuwa na mwanzo mzuri, mazungumzo yetu na Rais Kenyatta na Naibu wake Ikulu hayakuwa mabaya, tumejadiliana kuhusu mustakabali wa masuala ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na swala la IEBC.”
TAARIFA YA IKULU
Muda mfupi baadaye taarifa ya Ikulu ilisema: “Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta leo (jana), alimkaribisha na kufanya mazungumzo na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Korea Kusini, Park Geun-Hye, aliyemtembelea Ikulu. Waziri Mkuu wa zamani, Prime Minister Raila Odinga naye alihudhuria hafla hiyo kwa mwaliko wa Rais.
Chanzo: Daily Nation
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :