Wafuasi 11 wa CORD, wakamatwa na silaha za jadi, wakeielekea Uhuru Park

No comments
Wednesday, June 1, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Watu 11 wametiwa mbaroni na Polisi wakiwa na silaha za jadi mapema leo, katika uwanja wa Uhuru Park, Jijini Nairobi ambako Muungano wa Upinzani (CORD) unaoongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani, Raila Odinga, umepanga kufanyia maadhimisho ya sherehe za Madaraka Day. 
Sherehe za kitaifa zinafanyika mjini Nakuru katika uwanja wa Afraha ambapo Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kuwaongoza Maelfu ya Wakenya kuadhimisha siku hii muhimu katika Kalenda ya Jamhuri ya Kenya.
Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, OCPD wa Kilimani, Peter Kattan amesema watu hao walitiwa mbaroni wakiwa wamepakia matatu wakielekea katika Viwanja hivyo na kuongeza kwamba watu hao 11, tayari wamepelekwa katika kituo cha Polisi cha Kilimani.
Ulinzi umeimarishwa Jijini Nairobi huku wafuasi wa CORD wakiruhusiwa kufanya mkutano katika viwanja vya Uhuru licha ya taarifa za hapo awali ambazo zilikuwa zikiwataka viongozi wa CORD kufanya mkutano wao kwingine.
Wakati huo huo, Kumekuwa na foleni kubwa katika mji wa Nakuru asubuhi ya leo wakati ambapo mji huo unajiandaa kuandaa maadhimisho ya 53 ya sherehe za Madaraka (Madaraka Day). maadhimisho hayo yanafanyika katika uwanja wa Afraha.
Barabara nyingi zinazoelekea katikati mwa mji, zilizfungwa katika harakati za kuimarisha ulinzi. Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Rift Valley, Wanyama Musyambu, hata hivyo watembea kwa miguu wanaruhusiwa kutumia barabara zote bila usumbufu.
Chanzo: Citizen Tv

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .