BRUCE LEE: Mkali wa Mapigano "Martial Arts"anayedaiwa kuwa fiti kuliko mwanaume yeyote yule
Posted in
Filamu
No comments
Tuesday, July 5, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
China inasadikika kulikuwa na siku maalum ya kuadhimisha siku yake. Kwa hiyo wakati Lee anazaliwa Novemba 27, 1940 ilikuwa ni mwaka wa kuadhimisha siku ya Dragon kwa mujibu wa kalenda ya kichina. Pamoja na kuzaliwa katika Hospitali ya Chinatown Jijini San Francisco, baba yake Lee Hoi- Chuen alikuwa Mchina asilia japo mama yake Grace alikuwa mchina anayeamini madhehebu ya Roman Katoliki kutokana na mzazi mmoja kuwa Mjerumani.
Lee na wazazi wake walirejea Hong Kong akiwa na umri wa miezi mitatu. Hiyo ikazua utata kuhusu uraia wake halali, kwa sheria za Marekani wakati huo kwa kuwa alizaliwa nchini humo, moja kwa moja alikuwa mmarekani lakini pia wachina walidai kuwa raia wao na Hong Kong pia.
Baba yake Bruce Lee alikuwa miongoni mwa watu waliofanya kazi za sanaa kama kuimba wakisafiri kati ya China na mji wa Canton uliokuwa Hong Kong na pia alikuwa ni mcheza filamu hivyo ikamfanya awe akisafiri mara kwa mara.
Alifanya safari zake za muda za kutumbuiza katika jamii ya wamarekani waliolowea China baada ya uvamizi wa Japan katika vita ya Pili ya Dunia. Kusafiri na kutumbuiza sehemu mbalimbali ilikuwa biashara nzuri na iliyomlipa Lee ndipo aliposafiri tena Marekani na kupiga kambi kwa muda mrefu.
Hata hivyo pamoja na ndugu zake wengine kuendelea kukaa Marekani, Lee aliamua kurudi Hong Kong baada ya mkewe kujifungua mtoto wa nne. Hong Kong ikavamiwa na Japan na kumfanya Lee aishi miaka 3 na miezi minane katika uaktili mkubwa wa utawala wa Japan. Hata hivyo familia yake iliweza kupona na vita. Baadaye Lee Hoi-Chuen akaendelea na uigizaji wake filamu na kufanikiwa zaidi, wakenda tena Marekani hadi alipomzaa Bruce.
Mama yake Bruce Lee, Grace alikuwa mtoto wa tajiri mmoja wa Hong Kong aliyekuwa na nguvu Ho Tungs, alikuwa ni Rockfellers wa Hong Kong. Mama yake alikuwa ni binamu wa Sir Robert Ho Tung kutoka ukoo wa wa wenye pesa na alijikuta akikua katika maisha ya kifahari.
Baba yake Bruce Lee alikuwa miongoni mwa watu waliofanya kazi za sanaa kama kuimba wakisafiri kati ya China na mji wa Canton uliokuwa Hong Kong na pia alikuwa ni mcheza filamu hivyo ikamfanya awe akisafiri mara kwa mara.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :