MUAVI: "SENSA YA MAENDELEO TUJITOKEZE KUHESABIWA"
Posted in
No comments
Monday, June 25, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
IKIWA zimesalia chini ya mwezi mmoja tu kabla ya sense
ya mwaka huu kufanyika, jamii imeaswa kushiriki kikamilifu katika tukio hilo la
kihistoria nchini kwani ndio njia pekee ya kuirahisishia serikali kazi ya
kupanga mipango ya maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na mratibu wa sense mkoani Kilimanjaro
Alex Muavi akiongea na KIJIWEBLOG mara baada ya kuhudhuria kikao cha kamati ya
ushauri ya mkoa, RCC iliyofanyika hivi karibuni katika ofisi ya mkuu wa mkoa wakati
akizungumzia maandalizi ya timu ya sensa katika kuhakikisha kuwa zoezi hilo
linafanikiwa kama ilivyopangwa.
Muavi alisema timu ya sense hasa mkoani hapo iko
tayari kuhakikisha kila raia anapata haki yake ya msingi ya kuhesabiwa na
kuingizwa kwenye orodha ya serikali.
“Timu yangu haina mashaka kabisa , tumejiandaa, kila
kitu kikosawa ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata fursa ya kuhesabiwa
na kuingia kwenye daftari la kumbukumbu,” alisema Muavi.
Alisema shughuli
itaenda kama ilivyopangwa na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wamejipanga
kuhakikisha makosa yaliojitokeza katika sensa ya awali hayajitokezi tena.
“Tutahakikisha tunatenda haki katika kwa kila mtu na
nadhani kama mambo yatakwenda kama tulivyopanga, basi yale mapungufu yote
yaliyojitokeza katika sensa ya mwaka 2000 hayatajitokeza tena,” alifafanua
Muavi.
Alitoa wito kwa watanzania wote hasa jamii ya
wafugaji wa kuhamahama, wafanyabiashara na wafanyakazi kuwepo majumbani siku ya
tukio, ili kutoa nafasi kwa timu ya sensa kufanikisha kazi yake.
“Ndugu zangu wafugaji wa kuhamahama, wafanyabiashara
na wafanyakazi wengine kama mimi ni vyema tukatenga muda wetui na kutulia
majumbani ili kushiriki katika zoezi hili la kihistoria,” alisem,a Muavi.
Sensa ya mwaka huu ambayo kauli mbiu yake ni “sensa
ya maendeleo jiandae kuhesabiwa” ni sensa ya 5 kufanyika tangu uhuru na
inafanyika takribani miaka 12 tangu ilipofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2000.
MWISHO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :