Jeshi kuchunguza madai ya mauaji Mali

Posted in
No comments
Friday, January 25, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Mwanajeshi wa Kifaransa akiwa amesimama karibu na kifaru mjini Niono 20 Januari
Jeshi la Mali limesema kuwa litachunguza madai kuwa wanajeshi wamewaua raia wasio na hatia katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kiisilamu la Kaskazini
Afisaa mkuu wa jeshi aliambia BBC kuwa kwa sasa hawezi kuthibitisha au kukanusha n kuwa mauaji yalifanyika.
Shirikisho la kimataifa la kutetea haki za binadamu hapo jana lilituhumu wanajeshi wa Mali kwa kuwaua waarabu na watu wa jamii ya Tuareg ambao ni wachache.

Kwingineko, moja ya makundi ya wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa Mali, limegawanyika na kusema linataka kufanya mazungumzo.
Ni kwa mujibu wa taarifa za shirika la habari la AFP lililoweza kutupia jicho taarifa ya wapiganaji hao.

Vuguvu la (Islamic Movement for Azawad,) lilisema kuwa linajitenga na kundi zima la Ansar Dine, na linapinga vitendo vyote nvya kigaidi au siasa kali.
Kulingana na taarifa hiyo, kundi hilo linaongozwa na Alghabass Ag Intalla, kiongozi muhimu katika eneo la Kidal. Kidal.

Ufaransa ilituma kikosi cha jeshi, mapema mwezi huu ili kujaribu kukomesha harakati za makundi hayo.
Ilisema kuwa baadhi ya wapigananaji wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda, na baadhi yao wakiwa wageni, walitishia kugeuza Mali kuwa taifa la kigaidi.

Na katika harakati zinazoendelea dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu, mapema leo,watetezi wa haki za bibadamum, wamedai kuwa jeshi la Mali limewaua “kiholela watu kadhaa” katika harakati za kujaribu kuteka tena eneo la kaskazini lililoko chini ya mamlaka ya wapiganaji wa Waisilamu.

Shirikisho la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu, FIDH, limesema kwamba watu kadhaa waliuwawa kwa ajili tu walikuwa hawana vitambulisho.
Lakini mwanajeshi mmoja wa Mali alinukuliwa akikanusha madai hayo.
Madai mengine kuhusu mauaji ya kiholela pia yameripotiwa katika maeneo mengine ya magharibi na kati mwa nchi hiyo.

Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Ansar Dine
Habari zinazosema kwamba jeshi hilo, ambalo wengi wao ni Waafrika weusi kutoka kusini mwa nchi, wamekuwa wakiwalenga Waarabu na Watuareg kutoka kaskazini, jambo linaloashiria ubaguzi wa rangi katika mapigano hayo, ubaguzi ambao umefichwa na kuwepo kwa vikosi kutoka nchi za magharibi wanaopambana na wanamgambo Kiisilamu, Mark Doyle wa BBC aliyeko Mali alisema. 

'Uongo mtupu’
Shirika hilo la kutetea haki lilisema kwamba ni sharti kuwe na uchunguzi huru dhidi ya dhuluma hizo zilizofanywa na wanajeshi wa Mali, na kwamba wote waliotekeleza mauaji hayo wafaa waadhibiwe.

Katika kambi ya kijeshi mjini Sevare, takriban watu saba waliuwawa karibu na kituo cha basi na hospitali, shirika hilo lilisema.
Kuna “habari za kuaminika” kwamba watu wengine 20 waliuawa Sevare, huku miili yao "ikizikwa haraharaka, hususan katika visima. Kuna madai mengine kwamba mauji yangali yanaendelea", shirika hilo lilisema.
Mauaji kama hayo pia yalifanywa katika miji ua Mopti na Niono.
Washirika
Lilizidi kusema kuwa waathiriwa walishtakiwa kwa kuwa na silaha, na kwa kuwa "washirika" wa wanamgambo hao.

Nyumba za makumi ya Watuareg walioko Bamako, mji mkuu wa Mali, zimevamiwa na wanajeshi.

Capt Modibo Traore wa jeshi la Mali alisema kwamba madai hayo "yalikuwa uongo mtupu”, lakini akakataa kufafanua zaidi, shirika la habari la AP liliripoti.

Wakimbizi
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema kwamba raia 7,100 wameshatorokea nchi jirani tangu Jaunuari 10 January ili kuepuka mapigano hayo.
Afisa wa Umoja wa Mataifa Valentin Tapsoba alisema kwamba watu 7,100 walikuwa wametorokea nchi jirani katika majuma mawili yaliyopita. Wengi wao - 4,000 – walitorokea Mauritania, alisema.

Aliongezea kwamba wengine 3,100 walikuwa wamevuka hadi Burkina Faso na Chad, mashariki mwa Mali.
Takriban watu 10,000 wamehamia makambi ya wakimbizi nchini Mali tangu 10 Januari, alisema.
Wakimbizi walioko kambini mjini Sevare
Mzozo huu wa hivi karibuni ulizuka baada ya wanamgambo kuanza kuelekea kusini, wakishambulia miji ya Konna, Diabaly na Douentza iliyoko katikati mwa nchi. 

Ufaransa
Ufaransa ilituma wanajeshi wake mnamo 11 Januari ili kukwamisha hatua za wanamgambo hao.

Ilisema kwamba waasi hao, wenye uhusiano na al-Qaeda – na ambao wengine wao si Wamali – walikuwa wametoa tishio kwamba wataigeuza Mali kuwa "nchi ya magaidi".

Maafisa wa Ufaransa wamesema kwamba wanajeshi wao wamewasaidia wanajeshi wa Malia ili kuteka tena miji hiyo mitatu.
Ufaransa inategemea kuipa nchi ya Afrika Magharibi uongozi wa majeshi hayo ya pamoja, idadi ambayo kwa sasa ni 1,000.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .