Vurugu zatokea katika siku ya Maadhimisho Misri
Posted in
No comments
Friday, January 25, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Vurugu limezuka kati ya maafisa wa polisi na raia wa misri waliokusanyika katika Medani ya Tahrir mjini Cairo.
Leo ni maadhimisho ya pili tangu kufanyika
mapinduzi ya kiraia yaliyopelekea kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa
rais Hosni MubarakRaia wa misri wameshtumu vikali uongozi wa Raisi Mohamed Morsi na wafuasi wake wa chama cha Muslim Brotherhood kwa kuhujumu sababu ya mapinduzi hayo.
Upande wa upinzani umetaka kuondolewa kwa baadhi ya mabadiliko yanayotarajiwa kufanyiwa katiba mpya yaliyonakiliwa na bunge la nchi hiyo.
Bwana Morsi amekana madai hayo na kuitisha sherehe za amani.
Mahakama ya rufaa hivi maajuzi, ilibatilisha hukumu ya kifo dhidi ya Mubaraka kwa mauaji ya waandamanaji na kuamuru kesi hiyo kusikilizwa upya.
Mubaraka anasalia kizuizini katika hospitali ya jeshi.
Siku ya Alhamisi, jioni, polisi walikabiliana na wandamanamaji waliojaribu kuondoa vuzuizi barabarani, karibu na medani ya Tahrir.
Makabiliano hayo, yaliendelea usiku kucha huku polisi wakiwatawanya wandamanaji hao kwa kuwarushia gesi ya kutoa machozi. Takriban watu wanane walijeruhiwa.
Chama hicho hakijaitisha maandamano ya wafusia wake. Kinajianda kuadhimisha siku hii kwa kuzindua miradi ya kusaidia jamii.
Msukosuko wa kiuchumi
Kinatuhumu Morsi kwa kutumia nguvu pamoja na kuunda kwa haraka katiba inayopendelea waisilamu na hailindi haki za wanawake pamoja na wakristo.
Serikali hiyo pia imelaumiwa kwa kusababisha msukosuko wa kiuchumi.
Kabla ya maandamano ya leo, kiongozi mashuhuri wa upinzani Mohammed ElBaradei, alisema katika taarifa yake kuwa anatoa wito kwa kila mtu kujitokeza na kushiriki kwenye maandamano hayo, kuonyesha kuwa nia na lengo la mapinduzi lazima itimizwe.
Maandamano sawa na hayo yanaratajiwa kufanyika katika miji mingine ya Misri.
Rais amepuuza madai ya upinzani kama yasiyokuwa sawa na badala yake kuitisha mazungumzo.
Aidha Morsi, na wafuasi wake, wanatuhumu wapinzani wao kwa kuhujumu demokrasia kwa kukosa kuheshimu ushindi wa chama cha Muslim Brotherhood kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka mmoja uliopita.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :