MWANAFUNZI AJIUA KWA KUNYWA SUMU KILIMANJARO
Posted in
No comments
Thursday, January 31, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
MKAZI mmoja wa kijiji cha Weruweru, Maili sita
Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro,Hadji Yassin (16), ambaye ni Mwanafunzi wa kidato
cha pili katika Shule ya Sekondari ya mailisita, amefariki dunia baada ya
kunywa kitu kinachosadikiwa kuwa ni sumu.
Wakizungumza na MTANZANIA lililofika katika eneo la
tukio kwa masharti ya majina yao kutotajwa gazetini, baadhi ya mashuhuda ambao
pia ni ndugu wa marehemu, walisema kuwa waligundua kuwa ndugu ao amekunywa sumu
hiyo kutokana na kukuta chupa ya sumu
hiyo ikiwa kando yake na kumuwahisha katika Hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro,
Mawenzi.
“Tulimkuta ndugu yetu akiwa amelala na pembeni
kukiwa na chupa ya dawa ya wadudu shambani ya Serecrone, tulimpeleka Mawenzi
lakini kwa bahati mbaya, ndio hivyo tena,” alisema mmoja wa ndugu zake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa
Jeshi la Polisi mkoani Kilimamjaro, Robart Boaz alisema kuwa Marehemu alifariki
dunia majira ya saa 2:40 usiku wa Januari 30, katika hospitali ya Mawenzi alikolazwa
akipata matibabu.
Kamanda Boaz alisema kuwa hata hivyo uvchunguzi wa
chanzo na sababu za marehemu kufikia kuchukua uamuzi wa kusitisha uhai wake
bado zinaendelea na kuongeza kuwa Jeshi la Plisi linasikitishwa sana na matukio
kama hayo.
“Bado hatujafahamu ni kwa nini kijana huyu aliamua
kufanya hivyo, kwa kweli inahuzunisha
sana kuona vijana wakichukua maamuzi ya hatari kama haya, tunaendelea na
uchunguzi kubaini sababu za kijana mdogo kama huyu kukatisha maisha yake,”
alisema Boaz
Wakati huo katika Mtu mmoja alipoteza maisha usiku
wa jana, majira ya saa moja usiku, katika kijiji cha Maharo-Mamsera Juu, kata
ya Mamsera, wilayani Rombo, baada ya kugongwa na gari, namba za usajili T474
BHZ, Toyota Pickup, akiwa anavuka barabara kwa miguu.
Kamanda Boaz alisema kuwa tukio hilo lilitokea baada
ya mtu huyo aliyemtaja kwa jina la Jacob Shayo (46), aliyekuwa amepaki gari
lake, namba za usajili T367 BER, aina ya Mitsubishi Fuso na kukusudia kuvuka
barabara kwenda Ng’ambo ya pili kabla ya kugongwa na Gari hilo lililokuwa
likiendeshwa na Bernard Peter Mlingi, ambaye ni mkazi wa Tarakea Rombo.
Kamanda Boaz alisema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo
kasi kwani wakati tukio linatokea, dereva wa pickup lililogonga alikuwa
amepoteza mueleko na kumvaa marehemu ambaye alisema kuwa alifariki papohapo na
kuongeza kuwa mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hosptali ya Huruma,
wilayani Rombo.
MWISHO.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :