Gesi Mtwara ni vita
Posted in
No comments
Monday, January 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
WANANCHI WAUA POLISI, WACHOMA MAGARI 18, JK ATAKIWA KUKATISHA ZIARA
HALI ya
utulivu na amani mkoani Mtwara imetoweka baada ya baadhi ya wananchi
kuendeleza mapambano na serikali wakipinga gesi asilia iliyovumbuliwa
mkoani humo kusafirishwa kwenda Dar es Salaam bila kuwanufaisha wao
kwanza.
Vurugu hizo
zilizoibuka tena jana mkoani humo, zimeelezwa kuwa kubwa kuliko za juzi
zilizotokea mjini Mtwara, kwani watu wanne, akiwamo askari polisi,
wameuawa na wengine saba kujeruhiwa vibaya wakati polisi walipokuwa
wakipambana na waasi hao.
Vurugu za jana zilihamia wilayani Masasi ambako majengo ya serikali na ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliteketezwa kwa moto.
Mashuhuda wa
tukio hilo waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa chanzo cha fujo
hizo ni mzozo uliotokeza kati ya polisi na kijana mmoja mwendesha
pikipiki (bodaboda), ambaye anadaiwa kupigwa na askari.
“Wakati
mwendesha pikipiki akibishana na polisi, ilitokea hali ya kutoelewana,
hivyo polisi wakampiga kijana huyo na wakati wanampiga, mwenzake aliona
na kwenda kuwaita waendesha bodaboda wengine na kuibua vurugu kubwa
wakitaka kuchoma moto kituo cha polisi ili kulipa kisasi,” alisema
shuhuda wetu.
Kwa mujibu
wa shuhuda huyo, wakati waendesha bodaboda hao wakianzisha vurugu,
baadhi ya wananchi wa kawaida ghafla waliungana nao kuibua madai mengine
ambayo hayakuwa na uhusiano na madai ya waendesha bodaboda.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :