JK APOKEWA KWA SHANGWE KIGOMA, KUONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO LEO
Posted in
No comments
Sunday, February 3, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo
amepata mapokezi makumbwa mjini Kigoma mara baada ya kuwasili mkoani humo
kwaajili ya kuhudhuria kilele cha Maadhimisho ya miaka 36 ya CCM yanayo fanyika
kitaifa mkoani humo.
Rais
Kikwete aliyeambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma, Issa Machibya pamoja na viopngozi wengine wa Chama hicho akiwepo
Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti bara, Komredi Philip
Mangula, pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya chama hicho iliyokwisha
kutangulia mkoani humo juma lililopita kwa njia ya reli ya kati.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na viongozi wa mbalimbali wa chama hicho waliofika kumpokea.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mwigulu Mchemba.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na viongozi wa chama tawala ambao ni marafiki kutoka Congo DRC
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na makada na Wanachama wa Chama hicho Mkoani Kigoma kutoka Familia ya Saratoga.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na Mzee Mwilima.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akitazama
burudani ya ngoma kutoka kundi la Warumba Shauri la mkoani Kigoma. Anayepiga
Ngoma ni Mwajuma Hussein wa kundi hilo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :