MAJALIWA:"SERIKALI IMERUDISHA MICHEZO MASHULENI"
Posted in
No comments
Saturday, February 2, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
NAIBU WAZIRI TAMISEMI-KASIM MAJALIWA |
NAIBU waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa
(TAMISEMI), Kasim Majaliwa amesema serikali imeazimia kukuza michezo kwa kurudisha
michezo mashuleni.
Majaliwa aliyasema hayo katika mahafali ya 11 ya
shule ya sekondari ya Mkuu, wilayani Rombo baada ya kukabidhi zawadi kwa mwanafunzi
Fabian Swai (20), mwanafuzi wa kidato cha tano, aliyeibuka mchezaji bora kitaifa katika mashindano ya UMISETA 2012.
MAJALIWA KULIA AKIMSIKILIZA KATIBU MKUU TFF |
Majaliwa amesema kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha inaongeza ajira kwa vijana na njia mwafaka ni michezo kutokana na
ukweli kwamba sekta ya michezo ndio inayoongoza kwa kutoa nafasi za ajira duniani
kote kwa sasa.
Taasisi hiyo kwa mujibu wa Waziri Majaliwa inatoa
kozi kwa walimu kutoka vyuo 11 nchi nzima ambapo mpaka sasa zaidi ya walimu 388
kutoka katika shule za msingi na Sekondari wameshaanza kunufaika na kozi hiyo.
Majaliwa amesema kuwa kazi ya walimu hao itakuwa ni
kuzalisha wachezaji wenye kiwango katika ngazai za UMITASHUMTA na UMISETA, ili
hapo baadae wachezaji hao watumike katika timu mbalimbali za taifa.
Awali akitoa Taarifa kwa Naibu Waziri, Mkuu wa
Shule, Dickson Wandiba amesema kuwa Mwanafuzi Fabian,alifanikiwa kutwa medali mbili za dhahabu katika michezo ya
kurusha kisahani na kutupa tufe na medali moja ya shaba, katika mchezo wa
mkuki.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :