TFDA YATEKETEZA BIDHAA ZENYE THAMANI YA SH. MILIONI 38 MKOANI KILIMANJARO
Posted in
No comments
Wednesday, May 1, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Mwandishi wetu, Moshi
MAMLAKA ya
Chakula na dawa (TFDA) kanda ya kaskazini imeteketeza bidhaa mbalimbali
zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 38 vikiwemo vipodozi vyenye viambata vya
sumu.
Bidhaa zingine zilizoteketezwa ni dawa ambazo
zimepigwa marufuku na malmaka hiyo na ambazo hazijasajiliwa pamoja na vyakula
ikiwemo maziwa ya watoto.
Mkaguzi wa TFDA Kanda ya kaskazini Abdalla
Athman aliyaeleza hayo jana muda mfupi
baada ya kuteketezwa kwa bidhaa hizo katika kata ya Kaloleni mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Alisema bidhaa hizo wamezikamata wakati wa
ukaguzi ulioanza mkoani Kilimanjaro April Tatu hadi april 30 ambao ulifanyika
katika wilaya zote za mkoa huo.
Alifafanua kuwa katika bidhaa hizo
zilizokamatwa na kuteketezwa Vipodozi viko vya thamani ya Sh.Mil. 15,Vyakula
Mil. 15 na dawa za thamani ya Sh. Milioni Nane.
Alisema walifanya ukaguzi huo kwa lengo la
kukagua vipodozi hatarishi,madawa feki, usafi, usajili na vibali pamoja na hali
ya ubora wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa
wafanyabiashara.
Aidha Athmani
aliwatahadharisha wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi
kuhakikisha wanafuata utaratibu na waache kupita njia za pama hatua ambayo
itawawezesha kuepuka matatizo ya kuuza bidhaa feki na ambazo zimepgwa marufuku
na mamlaka hiyo.
“Niwaonye wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini
kutoka nje ya nchi, waache kupitisha njia za panya wafuate utaratibu,ili
kuepuka kukamatwa na bidhaa ambazo zimeingizwa bila kusajiliwa na ambazo
zimepigwa marufuku”alisema.
Akizungumza Dkt. Itikija Mwanga mkaguzi mwandamizi
wa dawa toka kanda ya mashariki alisema katika ukaguzi huo wamekamata dawa ya
mifugo aina ya Skazon ambayo ilishapigwa marufuku kutokana na kuonekana kuwa na
madhara kwa binadamu na kuwa kichocheo cha ugonjwa Kansa.
Alisema licha ya dawa hiyo na kupigwa marufuku na serikali kutumika kwa
mifugo kutokana na kuonekana kuwa hatarishi bado imekutwa ikiuzwa madukani
jambo ambalo ni hatari.
Kutokana na hali hiyo aliwataka wananchi kutoa
ushirikiano kuwataja wafanyabiashara ambao bado wanauza dawa hizo ambazo ni
hatari ili kufanikisha jitihada za mamlaka hiyo za kutokomeza kabisa dawa hizo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :