MTWARA KIMENUKA TENA!!!

Posted in
No comments
Friday, July 19, 2013 By danielmjema.blogspot.com



HALI ya mambo imeanza kuwa mbaya baada ya kuenea kwa habari kuwa baadhi ya wananchi wa mjini Mtwara waliivamia gari lililobeba mabomba ya gesi kutoka mjini humo.

Gari hilo lilikuwa limebaba mabomba hayo kutoka Mjini Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaamlimeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva wa lori hilo kujeruhiwa vibaya na kuibua taharuki. 


Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika Manispaa ya Mikinda Mtwara Mjini sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile kinacho dhihirisha kuwa wanamtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka kusafirisha gesi hiyo kwa ajili ya manufaa ya nchi. 

Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi  Mtwara, ikiwa
ni wiki moja tu imepita tokea watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka jijini Dar es Salaam kama ilivyokubaliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .