Kongamano la Nafasi ya Mtanzania Kumiliki Rasilimali za Taifa: Waziri Wa Nishati na Madini Mh Prof Sospeter Muhongo Atema Cheche
Posted in
No comments
Sunday, December 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri wa Nishati na Madini Mh Prof Sospeter Muhongo
---
Desemba 8,2013-Jumapili.UDSM
WAZIRI
wa Nishati na Madini Mh Prof Sospeter Muhongo ameona avunje ukimya na
kusema hadharani kuwa upotoshoji ukweli unaofanywa na watu wachache kwa
maslahi yao huku akimtolea mfano M/kiti wa TPSF, Bw Reginald Mengi ni
tatizo na kumtaja kumili ardhi yenye ukubwa wa 3886 sq km katika
machimbo na eneo la ukubwa wa 1300sq huku akisema ni sawa na Dar es
Salaam tatu.
Akielezea juu ya ulipaji kodi wa migodini Waziri Muhongo amesema," Mererani hawalipi kodi,
tunazo kampuni 597 kwa miaka 5 leseni zilizolipa mirahaba ni leseni 10
sawa na 32M/- wazee wa peeple's power naomba muwashughulikie hawa
kwanza."
Alieleza zaidi kuwa wachimbaji weusi yaani watanzania wapo 15 waliolipa kodi ni 10 tu. Aliongeza zaidi kuwa "...katika kampuni kubwa za nje hakuna kampuni inayofikia ukubwa wa maeneo kama wanayomiliki Watanzania ambao ni asilimia 70 na asilimia tano ndiyo joint venture, adui wa Watanzania ni Mtanzania mwenyewe."
Muhongo aliongeza kuwa kunawatu wanakatisha watu tamaa na kuwataka watu wanaotaka kumiliki vitalu waende ofisini kwake siku ya Jumanne ya keshokutwa asubuhi, na wawe wanauwezo wa kifedha"...na waje kwaajili ya kununua maeneo hayo kama hawana wasije".
Akionesha Mchanganuo wa fedha hizo alisema Mtu awe na USD10Milioni, pia USD Milioni 5 nyinginge,halafu katika mambo ya mazingira anatakiwa awe na USD 12Milioni, Uchongaji visima USD 510 nyingine, huku akisisitiza; Hizi hazitolewi benki, hizi zote unaweza kuwekeza bado ukakosa baada ya kuchimba yaani usipate ulichokitaka hiyo ni juu yako, Pia Uchimbaji wa tathimini ni USD 900Milioni na pia kuweka miundombinu kwa kutoa gesi baharini kwenda nchi kavu kunagharimu USD Bil115.
Alieleza zaidi kuwa Dira ya nchi ya mwaka 2025 ni kuwa Tanzania itakuwa katika GDP per capita ya Dolla 2000 kwa mtanzania wa hali ya chinina kuongoza kuwa ilikwenda huko tunahitaji umeme.
"Toka uhuru sasa hivi watanzania tumeongeza asilimia 21 toka 11 asilimia ya mwaka 2005 Rais Kikwete alipoingia madarakani," alisema Mh Muhongo na kuongeza kuwa. "Ili kuendana na dira ya nchi kufikia mwaka 2025 uchumi uliokuwa kwa asilimia 6.7 ni lazima ukue kwa asilimia 8 na lakini tunataka lazima ukue kwa 10 ndiyo dira yetu, na ili kufikia dira yetu lazima tuzalishe Megawatti 1500 za umeme zaidi."
Aliongeza kuwa "sasa tumemaliza kujadili juu ya sera sasa tunatengeneza sharia, raslimali za madini sasa zinaongeza mapato kwa asilimia 3.5 tunataka ikue na kufikia asilimia 10 kwa mwaka 2025," alisema Prof Muhongo.
Alimaliza kwa kusema kuwa "hii mijadala tunayoiendesha tujiulize tunaacha nini Mwl Nyerere aliacha nini kwetu, sisi wizara hatujakataa kumsaidia mtu asiendelee kiuchumi lah sisi tupo kwaajili ya wanyonge wa nchi hii."
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :