MTANZANIA AANGUA KILIO BAADA YA KUPOTEA NJIA UHURU MARATHON LEO
Posted in
No comments
Sunday, December 8, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wambura Lameck Ryoba ambaye alikuwa anaongoza kundi la watanzania wenzake katika mbio Uhuru Marathon, akiangua kilio baada ya kuingia uwanjani na kukuta mshindi akiwa tayari ameshatangazwa
|
Mwanariadha Wambura Lameck
Ryoba wa Holili Youth Athletics Club ameangua kilio baada ya kujikuta
akishindwa kufanya vizuri licha ya kuliongoza kundi la wafukuza upepo baada ya
kupotea njia kutokana na usimamizi mbovu wa mbio za Uhuru Marathon
zilizofanyika Jumapili ya Desemba 8, mwaka huu.
Wambura akizingumza kwa
masikitiko makubwa alisema kuwa alipotea njia kutokana na ukweli kwamba
hakukuwa na vibao maalum vya kuonyesha njia za kupita katika mbio hizo za
kilometa 5.
Aidha Mwanariadha huyo
anayechipukia alisema amekasirishwa sana na waandaji wa mbio hizo kutokana na
kutokuwa makini na wanariadha.
Pia Wambura alisema Waandaji
wanapaswa kujipanga tena msimu ujao kwa ajili ya mbio hizo kutokana na
changamoto ambazo zimejitokeza ikiwemo huduma ya maji kwa wachezaji haikuwa
nzuri kwa mbio zote.
Uhuru Marathon imemalizika kwa Elia
Daudi kutoka Arusha akimaliza katika nafasi ya 3 kwa kukimbia muda wa saa 1:07
akitanguliwa na wakenya wawili katika mbio za kilometa 21.
Kwa upande wanawake Mtanzania Jackline
Juma Sakili aliwainua watanzania baada ya kuongoza mbio hizo za kilometa 21 (Half
Marathon) kwa kukimbia saa 1:15:25 kwa hisani ya: http://holiliyouthathleticsclub.blogspot.com
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :