WANANCHI WAANDAMANA AFRIKA YA KATI KUSHINIKIZA RAIS AJIUZULU
Posted in
No comments
Friday, January 10, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Maelfu ya watu wamekimbia makwao kutokana na vurugu za kidini.Maelfu ya watu wanaandamana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumtaka Rais wa mpito nchini humo Michel Djotodia, ajiuzulu.
Baraza lote la mpito katika Jamuhuri ya Afrika ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika wanakutana kujadili mzozo wa taifa hilo unaoendelea.Mkutano huo wa viongozi wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa.
Lakini wajumbe kwenye mkutano huo wanasema walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni mkakati kuhusu mustakabali wa rais wa taifa hilo Michel Djotodia.Bwana Djotodia anakabiliwa na shinikizo kali kwa kukosa kusuluhisha mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchi humo kati ya wakristo na waisilamu, lakini msemaji wake amesema kuwa hawezi kujizulu.
Viongozi wa kikanda wanasema wajumbe mia moja na thelathini na watano waliitwa kwa mkutano huo kwa sababu ni raia wa nchi hiyo pekee wanaoweza kuamua hatma ya taifa lao.Ghasia baina ya wanamgambo wa kiislam na kikristo zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Djotodia aliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka jana hali iliyotumbukiza taifa hilo katika viya vya wenyewe kwa kwenyewe.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :