CHADEMA YAIBURUZA CCM KIBORILONI-MOSHI
Posted in
Siasa
No comments
Sunday, February 9, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
MGOMBEA wa Udiwani kata ya Kiboriloni kwa tiketi ya Chadema,Frank Kagoma ameibuka Mshindi katika uchaguzi huo uliuohusisha vyama vitatu, Chadema, CCM na UDP.
akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimazi wa Uchaguzi, Shaban Ntarambe alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki ambapo kutokana na kura zote zilizopigwa 1288, Kagoma ambaye ni Mwenyekiti wa kata ya Mnazi alipata kura 1019 dhidi ya kura 255 alizopata mpinzani wake wa karibu mgombea wa CCm, Willy Aidano.
Mgombea mwengine, Aidan Muganga Mnzava alijipatia kura 2 ambapo jumla ya kura halali zilikuwa ni 1276 na zilizoharibika ni 12.
Kulikuwa na vituo vikuu vitatu vya kupiga kura pamoja na vingine vidogo 11 na kufanya jumla ya vituo kuwa 14.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :