LEMBELI ATAHADHARISHA KUPOTEA KWA TEMBO NA NYUMBU KUFUNGWA KWA MASHOROBA TARANGIRE
No comments
Saturday, February 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mwandishi Wetu, Manyara
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ametahadharisha
kuhusu uwezekano wa wanyama wa hifadhi ya tarangire kutoweka kutokana na njia
ambazo hutumiwa na wanyama hao katika mizunguko yao kuzibwa kutokana na shuguli
za kibinadamu kama vile makazi na mashamba makubwa.
Lembeli
alitoa kauli hiyo juzi baada ya kupokea taarifa ya kiutendaji kutoka kwa Mhifadhi
wa hifadhi ya Tarangire, Steven Koli ambaye alisema wanyama hao kwa sasa
wamepungua mno kutokana na njia za mizunguko yao kuziba.
Awali
akitoa taarifa ya hifadhi kwa kamati hiyo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya
Tarangire, Steve Koli alisema kumekuwa na idadi kubwa ya watu katika maeneo
yanayozunguka hifadhi limeongeza mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo, makazi,
ufugaji na shughuli zingine za binadamu.
Koli alisema ongezeko hilo limesababisha kufungwa kwa baadhi ya shoroba (wildlife
corridors) ambazo ni njia za kupita wanyama, njia ambazo ni muhimu kwa ajili ya
wanyama wahamao hususan Nyumbu, Pundamilia na Tembo.
Lembeli
alisema wakati hifadhi hiyo inaanzishwa mwaka 1970, kulikuwa na jumla ya njia
tofauti 9 lakini kutokana na njia hizo kuzibwa hadi kufikia 3 wanyama hao waikuwa
ni 9 kwa sasa zimeonekana kuzibwa na
kufikia 3 tu kutokana na aidha ujenzi wa
makazi ya binadamu au mashamba makubwa.
Alisema
hifadhi zinategemeana na kwa maana hiyo wanyama huzunguka kwa kutumia njia
maalum, kwa mfano wanyama walioko tarangire wapo wanaotoka maeneo ya ngorongoro
na wengine wanakwenda kwenye maeneo ya simanjiro ambayo iko nje kabisa ya
maeneo ya simanjiro ambayo iko nje ya hifadhi.
“Sasa
kuna wimbi la hizo njia za wanyama kuzibwa, aidha kwa makazi ya binadamu au
mashamba makubwa hususan katika eneo hili, hali hii ni hatari kwa maisha ya
hifadhi zetu hapa nchini hasa hizi za kaskazini zote,” alisema Lembeli.
Alisema
Kama mzunguko unaowafanya wanyama wahame kutoka eneo fulani kwenda eneo lingine,
kwenda kuzaa au kutafuta watoto, itakakosekana, kuna hatari ya wanyama
kutotunga mimba na matokeo yake wanyama watakuwa,
watazeeka, watakufa na hakutakuwa na wanyama wengine.
“Jambo
hili ni jambo ambalo kuanzia serikali za mitaa, kwenye Halmashauri za wilaya na
kadhalika watambue umuhimu wa maeneo ya hifadhi za taifa, huu ndio urithi pekee
ambao tunaweza kuendelea kujivunia sisi watanzania, Tanzania inajulikana
duniani kote kwa uhifadhi wa wanyapori kwa watu wenye mapenzi mema wasiokuwa
wagomvi, kwa hiyo tuiendeleze,
“Ombi
letu na sisi katika ngazi ya bunge tutaendelea kuishauri serikali kwamba ni
muhimu sheria zilizoko zinazohusu shoroba zinazingatiwa,” alisema Lembeli.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :