SERIKALI YAKANA "VIJISENTI" VYA WABUNGE
Posted in
Matukio
No comments
Thursday, February 6, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCWQNvMd5_2rcNwxS72S_QzA9zLz-IXUHKXVCzQ8NG9dFFFzLdQdK3LiWgVQOtJXG5QE6_IegzSwiUaeQNzC4dzFEZIdCnDFnqUWoH6brUtggvcygyrtqkkVbtO-1K5pyiowggiffMqTE/s1600/jk.jpg)
Taarifa kutoka wizara ya fedha, imesema habari hiyo
ni ya upotoshaji kwa kuwa Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na
mwandishi yeyote kama inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.
Baada ya kuzuka kwa taarifa hizo
baadhi ya wabunge waliozungumza na vyombo vya habari walikiri kuwepo kwa
mipango hiyo huku wengine wakikanusha kuwa hawajawahi kupitisha
mapendekezo kama hayo bungeni.
Naye naibu spika wa Bunge la Tanzania, Job
Ndugai ameliambia shirika la habari la habari la Uingereza (BBC), kuwa habari hizo si za kweli '' nipende kusema kuwa
jambo hilo kwa kweli si la kweli.
Si la kweli kwa sehemu mbili, kwanza
kwa utaratibu wa utawala wetu bora Tanzania, hakuna mtu mwenye mamlaka
ya kujiongezea yeye mwenyewe kipato chake katika utumishi wa uma.kila
ambaye ana mshahara au marupurupu ya aina fulani lazima yaidhinishwe na
mamlaka au chombo kingine, ndio utaratibu wa utawala wetu.
Kwa hiyo na
sisi Bunge hatuna mamlaka ya kujipangia posho ya aina yoyoyte au
mshahara wa aina yoyote kwa wabunge au viongozi wa Bunge''.
Pia naibu spika Ndugai amesema madai ya baadhi
ya Wabunge kuwa kulikuwa na mpango huo si ya kweli na hayajawahi
kujadiliwa katika Bunge hilo.
Taarifa hizo zilisababisha malalamiko kutoka kwa
wananchi kuhusu hatua ya serikali kuwapatia wabunge kiasi hicho kikubwa
cha fedha huku ikidai kuwa haina fedha za kutekeleza miradi kwa ajili
ya huduma nyingine za umma.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :